Pre GE2025 Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu

Pre GE2025 Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.​

Leo nitazungumza mambo mawili mahususi ambayo sisi kama Chama tunaamini yanagusa Watanzania na yanazua taharuki na hofu, nitazungumza kuhusu sakata la wimbi kubwa la Viongozi wa CHADEMA, Watanzania wengine wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu na Vyomvo hivyo vikaendelea kukaa kimya, kuwateka Watu katika taratibu ambazo sio za kisheria, kutowafikisha Vyombo vya Kimahakama kwa utaratibu wa kisheria na wengine kuuawa”

“Tumeamua tupaze sauti kuwataka wenye Mamlaka Nchini kutambua kwamba thamani ya maisha ya kila Mtanzania mwenzetu ni kubwa kuliko chochote, kwahiyo sisi kama Jamii ya Tanzania ni wajibu wetu kusimama kuhakikisha haki kwa Watu wote inapatikana na tusiendelee kuruhusu baadhi Vyombo vya Dola viendelee kuwaua , kuwatesa na kuwapoteza Watanzania na sisi tukakaa kimya, lazima tuseme na tunasema kwa kujiamini na tunasema tukijiua kwamba athari zake ni nini hata kwa maisha yetu binafsi lakini lazima tuseme ili hatimaye ukatili huu usionekane kama ni mzaha au ngonjera”

“Siku za hivi karibuni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilitoka na tamko kuhusu kuongezeka kwa utekaji nyara, TLS walitoka na orodha kubwa ya Watu zaidi ya 80 kwa majina na maeneo waliyotoka, taarifa ya TLS imetoka August 09 mwaka huu ikionesha majina ya Watu waliotekwa na walipotekewa na wengine waliokutwa wamekufa katika vyumba vya kuhifadhi maiti, inapotoka taarifa hii halafu Vyombo vya Dola vikakaa kimya ili ni jambo ambalo limetulazimisha sisi kuungana na TLS kupasa sauti


Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
 
Historia :

Vikosi vya Hitler vya SS , Gestapo na Ujerumani ya Mashariki STASI viliogopwa sana ndani ya mifumo rasmi ya Polisi, Usalama wa Taifa na Jeshi lakini hatimaye SS, GESTAPO na STASI vilisambaratishwa pale kulipopatikana uongozi mpya madhubuti kupinga uwepo wa jeshi ndani ya jeshi.

Gestapo - Hiki kilikuwa kikosi cha polisi cha siri cha Wanazi . Kazi yake ilikuwa kufuatilia umma wa Wajerumani wenye dalili za upinzani au upinzani dhidi ya utawala wa chama cha Nazi. Machawa walitumika kuvisaidiwa sana kutoa taarifa siri ikiwemo Wajerumani wa kawaida kuwatambulisha raia wenzao kwa vikosi hivi katili vilivyofanya kazi nje ya mfumo rasmi wa vikosi vya polisi na usalama .Huduma ya usalama (SD) - Hili lilikuwa shirika la kukusanya habari la SS.


1724324881620.png


Vikosi vya SS (Schutzststaffel)​

  • SS kilikuwa Kikosi cha Ulinzi cha Hitler ( walinzi).
    • Ilianzishwa mwaka 1925 BK na kuongozwa na Heinrich Himmler.
  • SS iliajiri Wajerumani wazalendo uchwara vijana wa chama tawala. Ilikuwa ni matarajio kwamba askari wa SS pia watapata watoto na wanawake wa wazalendo uchwara.
  • Wanajeshi wa SS walikuwa wamefunzwa sana na wenye nidhamu sana (hii ilikuwa sababu moja kwa nini Hitler aliwapendelea kuliko SA).
  • Walivaa sare nyeusi.
  • SS ilikuwa na wafanyakazi wa kutwa 90,000 na 'wafanyakazi wasio rasmi' 200,000, ambao walikuwa ni watoa taarifa wanaopitisha taarifa
 
Hotuba ya Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe Leo imewaacha Wakongwe wengi njia panda

Imebeba Ujumbe uliojificha ila Mungu wa mbinguni na atufanyie Wepesi

Enzi za Askofu Kulola na Shehe Yahya mambo Haya Freeman Mbowe angeyaanzia kwao kabla ya kwenda public

Hii ya Leo kali Sana 🐼
 
Hotuba ya Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe Leo imewaacha Wakongwe wengi njia panda

Imebeba Ujumbe uliojificha ila Mungu wa mbinguni na atufanyie Wepesi

Enzi za Askofu Kulola na Shehe Yahya mambo Haya Freeman Mbowe angeyaanzia kwao kabla ya kwenda public

Hii ya Leo kali Sana 🐼
Hata wewe kwa uzi huu umetuacha njia panda ungeweka minofu kidogo ili twende sawa.
 
Hotuba ya Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe Leo imewaacha Wakongwe wengi njia panda

Imebeba Ujumbe uliojificha ila Mungu wa mbinguni na atufanyie Wepesi

Enzi za Askofu Kulola na Shehe Yahya mambo Haya Freeman Mbowe angeyaanzia kwao kabla ya kwenda public

Hii ya Leo kali Sana 🐼
Na wewe umeona uendeleze kutuacha njia panda ya Tazara
 
Tunaposema CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala kidhalimu hatuwaonei ni kweli hakuna tofauti kati ya CCM na Bokoharam
 
Kiukwel Hali sasahiv imekuw mbaya,swala la usalam wa watu limekuw midomon t(siasa nyingi)angal watu wanaangamia.duh hii kitu kwel ni mchezo mchafu
 
Jeshi la Polisi linatakiwa
Chama kikubwa kinatoa tamko

TOKA MAKTABA:

19 Agosti 2024

Temeke Dar es Salaam , Tanzania

KUTOWEKA VIONGOZI WA CHADEMA MKOA WA WILAYA DSM KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA CHADEMA WATOA TAMKO


View: https://m.youtube.com/watch?v=nfBNEaVqMBE

Benito Mwapinga mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke akiongoa na waandishi wa habari kisha kubainisha viongozi Deusdedith Soka na wenzake walipigiwa simu tarehe 18 Agosti 2024 kutoka kituo cha polisi Changombe kuwa ....




Maoni ya wananchi :
N.B :

Jeshi la polisi linatakiwa kufumuliwa hasa ngazi ya SACP kwenda vyeo vya CP wastaafishwe wote.

Hii itasaidia kurejesha usimamizi wa nidhamu na utendaji wa walio chini yao kuzingatia kanuni na GPO ya polisi wanapotumwa askari kwenda kukamata watuhumiwa.

Kufumuliwa , kuanzia kwenye sheria ya uanzishwaji wake, ili baadhi ya majukumu yabadilishwe, badala ya kutumia maguvu kwa kila kitu, litoe huduma kwa jamii sio kila MTU aliitwa Polisi anarudi akiwa amekua kichapo, wakati ufike kwamba sheria ya uanzishwaji wa Polisi irekebishwe badala ya kuendelea kuwa Tanzania Police force , liwe Tanzania Police Services, maguvu yaomdolewe kwenye sheria ya police, wafanye kazi kwa weledi sio maguvu
 
Nchi yangu naita mara 3:
Tanzania
Tanzania
Tanzania
 
Tanzania Police force , liwe Tanzania Police Services

Hawana maofisa wenye weledi kama maofisa ya JWTZ / TPDF ambao hupitia mafunzo ndani na nje ya Tanzania.

Maofisa wa polisi wanaishia vyuo vya Kilwa Road Dar es Salaam na CCP Moshi. Huwezi kuona nchi za nje wakileta maofisa wao wa Polisi Tanzania kwa mafunzo. Ila kwa jeshi letu la wananchi Tanzania JWTZ / TPDF nchi nyingi zinatambua umahiri wa kozi wa maofisa zinazoendeshwa Tanzania na kutuma waje Tanzania.

Historia inatuonesha Nyerere alilifumua jeshi la Tanganyika na kuliunda upya mwaka 1964 baada ya kuwatimua wote walichosababisha askari waliochukua maamuzi mikononi mwao kitu alichoita Aibu ya Taifa, na hivyo kuunda jeshi jipya la JWTZ lisilo na makandokando ya kikoloni kama lile la Tanganyika 1964.

Na mpaka leo tunaona nidhamu iliyotukuka ya JWTZ / TPDF iliyosimamiwa na maofisa vizuri tangu kuundwa JWTZ :

Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ / TPDF​



  • Mwaka 1974 hadi 1975 ni Brigedia Jenerali Simon Nkwera
  • Mwaka 1975 hadi 1980 ni Luteni Jenerali Tumaineel Kiwelu
  • Mwaka 1980 hadi 1983 ni Meja Jenerali Imran Kombe
  • Mwaka 1983 hadi 1988 ni Meja Jenerali Martin Mwakalindile
  • Mwaka 1988 hadi 1994 ni Luteni Jenerali Tumainiel Kiwelu
  • Mwaka 1994 hadi 2001 ni Luteni Jenerali Gideon Sayore
  • Mwaka 2001 hadi 2006 ni Luteni Jenerali Iddi Gahhu
  • Mwaka 2006 hadi 2007 ni Luteni Jenerali Davis Mwamunyange
  • Mwaka 2007 hadi 2012 ni Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo
  • Mwaka 2012 hadi 2015 ni Luteni Jenerali Samweli Ndomba
  • Mwaka 2015 hadi 2017 ni Luteni Jenerali Venance Mabeyo
  • Mwaka 2017 hadi 2018 ni Luteni Jenerali James Mwakibolwa
  • Mwaka 2018 hadi 2021 ni Luteni Jenerali Yacoub Mohamed
  • Mwaka 2021 hadi 2022 ni Luteni Jenerali Mathew Mkingule
  • Mwaka 2022 hadi sasa ni Luteni Jenerali Salim Othman
Soma
Aibu ya Taifa ilivyotatuliwa kwa kufukuza askari wasio na nidhamu 1964,

Nini kinashindikana kulifanyia mageuzi makubwa jeshi la Polisi ili kuondokana na aibu ya taifa inayoikumba Tanzania kupitia jeshi la polisi 2024
 
Hii culture ya kishenzi ya kuteka watu na kuua ilianzishwa na Magufuli , system inabidi isafishwe na serikali ya CCM wakishindwa wengine wataisafisha tuu
 
Back
Top Bottom