Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Godbless Lema na Boniface Jacob waachiwa kwa dhamana

Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Godbless Lema na Boniface Jacob waachiwa kwa dhamana

Vibendera tayari mlisha pata lakusema
Yaani mpo kama makasuku tu
Makelele JF Na ID fake Kutoa Bitwe nje Hamna
 
Ila Mbowe Mungu atamlipia tu! utawala huu umemtesa kwanamna zote kana kwamba wao wataishi milele.
Mpaka sasa sijaelewa Magufuli anamfanyia Freeman Mbowe ukatili kwa manufaa gani! Nijuavyo Mimi Magufuli ni Rais wa Tanzania, kwa mjibu wa Katiba yetu na Biblia Rais ni mtawala kwa niaba ya Mungu kwa watu wote ndani ya Jamuhuri ya Tanzania. Magufuli kuamfanyia ukatili Freeman Mbowe ni kupingana na kanuni ya Mungu ambae daima huwatendea mema wema na wabaya wake. Ndo maana mvua haichagui kunyeshea mashamba ya watakatifu tu.
 
Ni baada ya kutishwa na Marekani, mashetani wakubwa hawa.
Walipokuwa ndani hukusema hivyo. Ulitaka waendelee kukaa ndani jua kuwa wanaumia wenzako kuna mbu balaa nilishawahi kukaa mkuu huko!
 
Utawala uliopita ulimbeba sana mpaka kupewa Kandarasi kadhaa kwny Hotels zake,

Matangazo ya Serikal kwny Magazeti yake na Kandarasi ya kubeba Vifurusho pale Kilimamjaro International Airport (KIA)

bila ya kusahau tangu 2006~2015 hakulipa hata Senti tano NHC kwa upangaji wake pale Bilicanus lakin Kina Nehemia walipokea maelekezo 'wasimbughudhi'

lakin ikawa Kila siku Matusi na kejeli kwa Jakaya hayaishi

Kila mchuma janga hula na wakwao

Ila Mbowe Mungu atamlipia tu! utawala huu umemtesa kwanamna zote kana kwamba wao wataishi milele.
 
Huyu Magufuli na huu utawala wake wa kiimla hauna future, tuko hapa.
 
Magufuli ajitafakari Sana Tena Sana Kama kweli anatumiwa na Mungu kuwaongoza watanzania au analazimisha! Nimeshauri kuingia kwenye maombi mazito kwa mwenyezi Mungu akiomba kufumbuliwa fumbo hili la uongozi ili afanye maamuzi magumu kwa faida ya taifa hili la Mungu!
Ageuke nyuma aangalie Kama kweli katika mikutano yake umati ule ulikuwa pale kwa hiyari yao ama la! Na Kama sivyo Basi ajue Hana ulazima wa kulazimisha kazi ya Mungu ya kuwaongoza Wana wa Mungu kwani kazi ya Mungu ni wito kutoka kwa Mungu mwenyewe! Aionee huruma nafsi yake!
 
Magaidi huwa wanapewa dhamana? Polisi ukipewa maelekezo tumia na akili zako.
Mkuu OKW BOBAN SUNZU ni wakati wa kujitafakari kama kweli upinzani ulikuwa na nafasi ya kushinda! Zifuatazo ni baadhi ya sababu, nyingi zimejadiliwa sana humu jamvini, ambazo kimsingi hao viongozi wasingekuwa na uhalali wa kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo, kushinikiza Uchaguzi Mkuu urudiwe:

√ Mbowe mwenyewe amekuwa akiamru wabunge wake wasusie vikao vya bunge, hasa vya bajeti. Wapiga kura walisikia na kuona;
√ Mbowe na karibu kundi zima la viongozi wa upinzani wamekuwa/wakaendelea kudai Serikali ya CCM ilikuwa inajishughulisha na maendeleo ya vitu. Wapiga kura wamewasikia, wakaona vitu (miundo mbinu na huduma za afya) jinsi vilivyonavyoboreshwa. Wamevitumia kiasi cha kuamini viongozi wa Serikali ya CCM. Kwenye sanduku la kura wapiga kura wameonesha imani hiyo;
√ Mbowe, huyo huyo, kama kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani, kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019. Hivyo basi Upinzani ukakosa wawakilishi kwenye Serikali za Mitaa, ambako ndiko kwenye nguvu ya ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu, 2020. Wagombea wao wakakosa msaada ngazi hiyo na kufanya kampeni kams watoto wakiwa. Upweke huo ukajibiwa kwenye sanduku la kura;
√ Ni Mbowe huyo huyo alishinikiza Lissu awe Mgombea wa Urais kupitia chama CHAKE, wakati akijua madhaifu yake. Wapiga kura wakahudhuria kampeni zake za majivuno, kero, matusi nk. Baada ya hapo wamemwadhibu kwenye sanduku la kura;
√ Viongozi wakuu wa CHADEMA na ACT-Wazalendo wakaingia kwenye Uchaguzi Mkuu na nia ya kisanii ya kuungana, kumbe nyuma ya pazia, Mbowe huyu huyu, ana agenda yake ya siri, kumtosa Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo. Wapiga kura (wanachama na wafuasi wa ACT-Wazalendo) wakasikia na kuona usanii huo. Kwenye kura wakamjibu Mbowe na kundi lake; na
√ Mgombea wa Urais, kupitia CHADEMA, alipofungiwa na NEC kutokuendelea na kampeni kwa siku kadhaa, Mbowe alijitokeza hadharani kulaani vyama vya upinzani vilivyoshiriki kupiga kura hiyo kuwa ni mamluki wa CCM. Viongozi wa vyama hivyo, wanachama na wafuasi walisikia, wakaona na kujibu kwenye sanduku la kura.

Uchaguzi Mkuu 2020, ulikuwa Huru na wa Haki kwa 100% kwa sababu kuu zifuatazo:
1) Wapiga kura walishiriki mchakato wote (kujiandikisha, kushiriki na kupiga kura) kwa uhuru kabisa na kutumia haki yao.
2) Wagombea nao kwa Uhuru, walitumia Haki yao kushiriki katika kinyang'anyiro hicho, kwa kuomba kuteuliwa na vyama vyao, kupitishwa na Tume, kufanya kampeni na hatimaye kushiriki wenyewe kupiga kura.

Kitendo cha viongozi hao kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo, sasa yanalaaniwa kila kona ya nchi na kila kundi katika jamii. Sasa ni wazi kuwa viongozi hao hawakuwa na nia njema katika Taifa bali wao kuingia madarakani kwa njia yoyote ile, ikiwemo umwagaji damu. Sheria za nchi, baada ya wananchi kuwaadhibu kwenye sanduku la kura, nazo zitawaadhibu.

cc: wafuasi wa upinzani humu JF
 
Magufuli ajitafakari Sana Tena Sana Kama kweli anatumiwa na Mungu kuwaongoza watanzania au analazimisha! Nimeshauri kuingia kwenye maombi mazito kwa mwenyezi Mungu akiomba kufumbuliwa fumbo hili la uongozi ili afanye maamuzi magumu kwa faida ya taifa hili la Mungu!
Ageuke nyuma aangalie Kama kweli katika mikutano yake umati ule ulikuwa pale kwa hiyari yao ama la! Na Kama sivyo Basi ajue Hana ulazima wa kulazimisha kazi ya Mungu ya kuwaongoza Wana wa Mungu kwani kazi ya Mungu ni wito kutoka kwa Mungu mwenyewe! Aionee huruma nafsi yake!
Who are you? Utopolo's comment!
 
Mpaka sasa sijaelewa Magufuli anamfanyia Freeman Mbowe ukatili kwa manufaa gani! Nijuavyo Mimi Magufuli ni Rais wa Tanzania, kwa mjibu wa Katiba yetu na Biblia Rais ni mtawala kwa niaba ya Mungu kwa watu wote ndani ya Jamuhuri ya Tanzania. Magufuli kuamfanyia ukatili Freeman Mbowe ni kupingana na kanuni ya Mungu ambae daima huwatendea mema wema na wabaya wake. Ndo maana mvua haichagui kunyeshea mashamba ya watakatifu tu.
Ficha upumbavu wako Ukatili upi
Mipanga aliyo kuwa akiifanya Ilikuwa mizuri
Nabado Wataelewa tu
Leo Akajipongeze na Faru John
 
Back
Top Bottom