Mkuu OKW BOBAN SUNZU ni wakati wa kujitafakari kama kweli upinzani ulikuwa na nafasi ya kushinda! Zifuatazo ni baadhi ya sababu, nyingi zimejadiliwa sana humu jamvini, ambazo kimsingi hao viongozi wasingekuwa na uhalali wa kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo, kushinikiza Uchaguzi Mkuu urudiwe:
√ Mbowe mwenyewe amekuwa akiamru wabunge wake wasusie vikao vya bunge, hasa vya bajeti. Wapiga kura walisikia na kuona;
√ Mbowe na karibu kundi zima la viongozi wa upinzani wamekuwa/wakaendelea kudai Serikali ya CCM ilikuwa inajishughulisha na maendeleo ya vitu. Wapiga kura wamewasikia, wakaona vitu (miundo mbinu na huduma za afya) jinsi vilivyonavyoboreshwa. Wamevitumia kiasi cha kuamini viongozi wa Serikali ya CCM. Kwenye sanduku la kura wapiga kura wameonesha imani hiyo;
√ Mbowe, huyo huyo, kama kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani, kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019. Hivyo basi Upinzani ukakosa wawakilishi kwenye Serikali za Mitaa, ambako ndiko kwenye nguvu ya ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu, 2020. Wagombea wao wakakosa msaada ngazi hiyo na kufanya kampeni kams watoto wakiwa. Upweke huo ukajibiwa kwenye sanduku la kura;
√ Ni Mbowe huyo huyo alishinikiza Lissu awe Mgombea wa Urais kupitia chama CHAKE, wakati akijua madhaifu yake. Wapiga kura wakahudhuria kampeni zake za majivuno, kero, matusi nk. Baada ya hapo wamemwadhibu kwenye sanduku la kura;
√ Viongozi wakuu wa CHADEMA na ACT-Wazalendo wakaingia kwenye Uchaguzi Mkuu na nia ya kisanii ya kuungana, kumbe nyuma ya pazia, Mbowe huyu huyu, ana agenda yake ya siri, kumtosa Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo. Wapiga kura (wanachama na wafuasi wa ACT-Wazalendo) wakasikia na kuona usanii huo. Kwenye kura wakamjibu Mbowe na kundi lake; na
√ Mgombea wa Urais, kupitia CHADEMA, alipofungiwa na NEC kutokuendelea na kampeni kwa siku kadhaa, Mbowe alijitokeza hadharani kulaani vyama vya upinzani vilivyoshiriki kupiga kura hiyo kuwa ni mamluki wa CCM. Viongozi wa vyama hivyo, wanachama na wafuasi walisikia, wakaona na kujibu kwenye sanduku la kura.
Uchaguzi Mkuu 2020, ulikuwa Huru na wa Haki kwa 100% kwa sababu kuu zifuatazo:
1) Wapiga kura walishiriki mchakato wote (kujiandikisha, kushiriki na kupiga kura) kwa uhuru kabisa na kutumia haki yao.
2) Wagombea nao kwa Uhuru, walitumia Haki yao kushiriki katika kinyang'anyiro hicho, kwa kuomba kuteuliwa na vyama vyao, kupitishwa na Tume, kufanya kampeni na hatimaye kushiriki wenyewe kupiga kura.
Kitendo cha viongozi hao kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo, sasa yanalaaniwa kila kona ya nchi na kila kundi katika jamii. Sasa ni wazi kuwa viongozi hao hawakuwa na nia njema katika Taifa bali wao kuingia madarakani kwa njia yoyote ile, ikiwemo umwagaji damu. Sheria za nchi, baada ya wananchi kuwaadhibu kwenye sanduku la kura, nazo zitawaadhibu.
cc: wafuasi wa upinzani humu JF