Makampuni makubwa duniani yamekuwa yakitumia fedha nyingi kujitangaza na kutangaza bidhaa zao ili kupata watumiaji/walaji wengi zaidi,huku yakishindana katika kutoa bidhaa bora na zitakazoshindana na zingine.Kila kampuni ina nembo yake(Logo) ambayo inatumika kama utambulisho wa bidhaa au kampuni husika.Nembo hizi(Trade marks)hazitambulishi kampuni tu na bidhaa zake, bali hata filosofia na mrengo(affiliation) wa kampuni yenyewe.Orodha ifuatayo ni makampuni yenye nembo/trade mark zilizo na uhusian wa kipagani,kichawi na kishirikina.
1.ALFA ROMEO
Kampuni la utengenezaji magari lenye makao makuu yake Milan Italia.Alfa Romea wamekuwa ni watengenezaji wazuri sana wa magari ya kifahari.Nembo ya Alfa Romeo kwa kifupi ni ya kutisha! ni Duara mabalo ndani yake kuna joka kubwa linaloonekana likimeza mtu alinyoonya mikono yake juu kwa woga.Wote tunajua nyoka anamaanisha nini...sio tu katika vitabu vya dini,hata katika maisha ya kawaida nyoka ni kiumbe kinachohusishwa na uouvu,kifo na mikosi.Kampuni linapoamua kutumia joka linalomeza mtu kama nembo yake lina maana ya kichawi/kishirikina au kipagani iliyo jificha.
2,APPLE MACKINTOSH.
Hili ni moja kati ya makampuni makubwa ya computer na yenye kutengeneza bidhaa zenye ubora uliotukuka.Nembo ya kampuni hii ni tunda aina ya apple lililong'atwa na kunyofolewa kipande.Wachunguzi wa mambo ya kipagani nia kishirikina wanahusisha nembo hii na kitendo cha kula tunda la mti wa uzima kama Adam na Eva walivyofanya katika bustani ya Eden..."The forbiden fruit" kama vitabu vya Mungu vinavyotanabaisha.Symbollically logo hii ni kama inasherehekea anguko la Adam na Eva katika bustani ya Eden baada ya kula tunda lile na kumuasi Muumba wao.Ikumbukwe kuwa kampuni hii ilianzishwa na Steve Jobs na Steven Wozniak miaka ya 70 na computer yao ya kwanza walioipa jina la Apple 1 waliiuza$ 666.66.Kama tujuavyo namba 666 imeandikwa katika vitabu vya Mungu kama alama ya Mnyama."beast" na mshirika mkubwa wa shetani.
3
,VODAFONE.
Vodafone....moja kati ya makampuni makubwa sana duniani lenye makao yake makuu Newbury Uingereza.Logo ya Vodafone inaingia katika kundi hili kwa kuwa na namba 6 tatu kama "MARK OF THE BEAST" ama alama ya mnyama au namba ya Shetani-Lucifer kama inavyotamkwa katika vitabu vya dini.Wenye kampuni hii waeona ni jambo la maana tu kujitwika nembo hii na namba hizi kama inavyoonekana hapo chini....
4,WALT DISNEY
Hili ni kampuni la vikaragosi maarufu na utengenezaji picha za filamu lililobuniwa na
Walter Elias "
Walt"
Disney ambalo kwa mwaka 2010 lilingiza kiasi cha dola bilion 36.Kampuni hii pia kama ilivyo vodafone hapo juu..nayo imetumia namba 666 iliyojificha.Angalia logo ya disney hapo chini...
5,EXXON MOBIL
Exxon Mobil kutoka Marekani labda ni kampuni kubwa la mafuta na gesi kuliko yote duniani in terms of capital na faida.Kampuni hii ina nembo ya kukufuru ikionyesha misalaba miwili, tena kwa msisitizo yenye rangi nyekundu ili walaji/watumiaji wa bidhaa za kampuni hii wajue tu "who is the boss" hapa."Fallen cross" ni alama inayotumiwa sana na wapagani kukashifu na kutukana ukristo na kudhihaki kifo cha Yesu msalabani.Alama hii imekuwa ikitumika sana na waabudu mashetani katika "black mass" mara nyingi.Tazama nembo ya Exxon hapo...
6 CBS
CBS ni moja kati ya mashirika makubwa sana ya utangazaji..si tu Marekani..bali duniani kote.Nembo ya CBS kama inavyoonekana hapo chini ni jicho moja.Jicho hili linalojulikana zaidi kama
"The all -seeing eye of Horus" ni moja kati ya nembo za kipagani zinazotumika sana na makampuni makubwa duniani huku wakibadilisha kidogo tu muonekano wa jicho hilo.Horus ni 'mungu' aliyekuwa akiiabudiwa sana Misri ya kipagani na Mafirauni kabla ya kuingia kwa ustaarabu ciwa uisilamu huko.Alama hii ya jicho la Horus inatumika sana na hata katika 1 dollor bill. Jicho hili pia limetumika..jicho hili katika dola moja....
HITIMISHO
Dunia imekuwa ikiendeshwa kishirikina mno na ikumbukwe kuwa mambo haya yalianza zamani sana.Makampuni makubwa yamekuwa yakitumia nembo au namba za kishirikina na kipagani kutoka katika miungu ya zamani ya Misri na Babeli katika bidhaa zao yakiiamini kuwa nembo au namba hizo zina nguvu za ajabu.Kwa mtazamo wa haraka utaona kwamba makampuni haya ni makubwa na yamefanikiwa sana kibiashara na kifedha.Lakini ikumbukwe kwamba utumiaji wa nembo hizi katika bidhaa zao ni kielelezo cha filosofia na mrengo wa makampuni husika katika maswala ya kiimani na mahali yalipojiegemeza
(Sartanism)