mkandi
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 281
- 121
Maxence,
Lakini naomba nikufahamishe kidogo kuhusiana na alama ya nyoka anayening'inia kwenye mti. Nyoka yule anayening'inia kweny mti kwanye logo ya Muhimbili ni replication ya kwenye Biblia baada ya Musa kumwinua nyoka wa shaba na kumtundika mtini ambapo kila mtu aliyeng'atwa na nyoka za sumu zilizotumwa kuwaua Waisraeli baada ya kuabudu sanamu badala ya Mungu na kufanya uzinzi pale jangwani. Kila mtu aliyeng'atwa na akamwangalia nyoka wa shaba aliyetundikwa mtini alipona.
Nadhani hiyo ndiyo rationale ya yule nyoka kwenye logo ya Chuo cha Tiba Muhimbili.
Mwanzoni niliwahi fikiri hivyo. Lakini kwa sasa najua kua ni alama ya mnyoo aitwae kitaalam Wuchereria bancrofti anaesababisha matende (filariasis). Mnyoo huyu kabla ya kudhibitiwa, aliuutesa sana ulimwengu wa afya, kabla ya tiba yake. Na ndo sababu ya kuepo hiyo alama. Sio Muhimbili tu, ila angalia nembo zote kunako medical professional.