Friji yangu inawaka na kuzima, tatizo litakuwa nini?

Friji yangu inawaka na kuzima, tatizo litakuwa nini?

Mpatuka

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2015
Posts
2,261
Reaction score
3,580
Friji langu aina ya Boss linawaka na kuzima. Ukiwasha linafanya kazi kwa dakika takribani mbili Kisha linazima kwa dakika kadhaa, halafu linajiwasha tena. Hivyo ndugu zangu waliowahi kukutana na changamoto hii naombeni msaada tafadhali?
 
Umelinunua lini? Seems like huna uzoefu na friji inavyofanya kazi. Kujizima na kujiwasha ni process la friji lenyewe
We cha kufanya likijizima, fungua mlango wa chini kama taa inawaka, then leta mrejesho.
 
Duh sidhani kama ni tatizo hilo.fridge ni kama pasi Kuna Mahali baridi ikifika kiasi Fulani linajizima.Hapo huna haha ya kuchomoa au kuzima kwenye switch coz muda wote linajibalance
Awali lilikuwa linafanya hivyo ila si kwa kuwaka na kuzima kwa dakika chache. Lilikuwa linatumia muda mrefu kidogo, linawaka kwa zaidi ya saa kisha linazima kwa dakika kadhaa. Lakini sasa hivi linafanya hivyo ndani ya dakika 5 tu kujiwasha na kuzima hali ambayo siyo ya kawaida kabisa.
 
Awali lilikuwa linafanya hivyo ila si kwa kuwaka na kuzima kwa dakika chache. Lilikua linatumia muda mrefu kidogo, linawaka kwa zaidi ya saa kisha linazima kwa dakika kadhaa. Lakini sasa hivi linafanya hivyo ndani ya dakika 5 tu kujiwasha na kuzima hali ambayo siyo ya kawaida kabisa.
Una tabia ya kulizima wewe kama wewe?

Kama hamna itakuwa lishapata baridi ndio maana linajizima
 
Umelinunua lini? Seems like huna uzoefu na friji inavyofanya kazi.

Kujizima na kujiwasha ni process la friji lenyewe
We chakufanya likijizima, fungua mlango wa chini kama taa inawaka, then leta mrejesho
Lina mwezi tu, nimelifungua taa inawaka kama kawaida. Kinachonishangaza hapo awali lilikuwa likitumia muda kufanya hivyo. Lakini kwasasa linajiwasha na kujizima within 5 to 6 minutes
 
Lina mwezi tu, nimelifungua taa inawaka kama kawaida. Kinachonishangaza hapo awali lilikua likitumia muda kufanya hivyo. Lakini kwasasa linajiwasha na kujizima within 5 to 6 minutes
Ubaridi uliopo unatosha, thermostat inafanya kazi.
 
Lina mwezi tu, nimelifungua taa inawaka kama kawaida. Kinachonishangaza hapo awali lilikua likitumia muda kufanya hivyo. Lakini kwasasa linajiwasha na kujizima within 5 to 6 minutes
Je kazi yake ya kupoza linafanya au linazima tu vitu vikiwa na hali yake ya kawaida bira ubaridi wala kupoa? .
Ongeza nyama kidogo tupate pa kuanzia ,
 
Lina mwezi tu, nimelifungua taa inawaka kama kawaida. Kinachonishangaza hapo awali lilikua likitumia muda kufanya hivyo. Lakini kwasasa linajiwasha na kujizima within 5 to 6 minutes

Mbona sio dakika nyingi 5 to 6 minutes nilijua lisaa limoja,

Swali la msingi linapata ubaridi achana na kujizima
 
Awali lilikuwa linafanya hivyo ila si kwa kuwaka na kuzima kwa dakika chache. Lilikua linatumia muda mrefu kidogo, linawaka kwa zaidi ya saa kisha linazima kwa dakika kadhaa. Lakini sasa hivi linafanya hivyo ndani ya dakika 5 tu kujiwasha na kuzima hali ambayo siyo ya kawaida kabisa.
😀 😀 😀 😀shule shule shule...!! labda kama halina ubaridi wa mabarafu sehemu ya freezer. ila friji ndivyo linavyofanya kazi
 
La kwangu upande wa Fridge halina ubarid kabisa,ila upande wa Frizer kule juu liko poa kabisa..ni takribani wiki sasa. Kama kuna fundi anisaidie changamoto ni nini.
 
Nina fridges mbili zinatatizo Kama lako, nilileta fundi akaniambia tununue kifaa elfu 30k moja ikatulia, baadae likarudia tatizo.

Baadae nikapata mafundi wengine wakaomba 50k zikakaa sawa, ndani ya siku kadhaa, matatizo yakawa mengi. Fridge moja ni mtumba lingnie nilichana mwenye kwa boz brand Boss.

Mtoa mada, tatizo lako ni kama langu, labda utafute mafundi wazoefu wanaweza kukusaidia.
 
Awali lilikuwa linafanya hivyo ila si kwa kuwaka na kuzima kwa dakika chache. Lilikua linatumia muda mrefu kidogo, linawaka kwa zaidi ya saa kisha linazima kwa dakika kadhaa. Lakini sasa hivi linafanya hivyo ndani ya dakika 5 tu kujiwasha na kuzima hali ambayo siyo ya kawaida kabisa.
Unatumisa fridge guard? Kama ndio jaribu kuitoa huwa zinazingua nilikuwa na tatizo kama hilo nikabadilisha fridge guard kesi ikaisha.

Jaribu kuwasha bila fiji guard
 
Awali lilikuwa linafanya hivyo ila si kwa kuwaka na kuzima kwa dakika chache. Lilikua linatumia muda mrefu kidogo, linawaka kwa zaidi ya saa kisha linazima kwa dakika kadhaa. Lakini sasa hivi linafanya hivyo ndani ya dakika 5 tu kujiwasha na kuzima hali ambayo siyo ya kawaida kabisa.
Hiyo sio kawaida, unaweza kuta una tatizo la compresor
 
Je kazi yake ya kupoza linafanya au linazima tu vitu vikiwa na hali yake ya kawaida bira ubaridi wala kupoa? .
Ongeza nyama kidogo tupate pa kuanzia ,
Linapoza mkuu ila kilichonipa wasiwasi ni time range tu ilivyobadilika.
 
Back
Top Bottom