Friji yangu inawaka na kuzima, tatizo litakuwa nini?

Friji yangu inawaka na kuzima, tatizo litakuwa nini?

Haka kadude nimetupia kabatini
 
Attachments

  • 20230307_173748.jpg
    20230307_173748.jpg
    460.8 KB · Views: 20
Langu ni Hisense
Sina guard
Huko dukani waliniambiaga hayo yana guard ndani kwa ndani.

Niko safe wakuu?
Naliwasha muda karibu wote.. nazima siku ya kulisafisha

Nunua guard mkuu
 
Boss ziko vyema...yangu mwaka wa tatu inaenda
Hakuna tatizo
 
Mkuu, angalia hapa kwenye hii switch, Zungusha weka namba 5. Itagandisha barafu hadi ushindwe kupasua hiyo barafu.
moja.jpg
 
Lina mwezi tu, nimelifungua taa inawaka kama kawaida. Kinachonishangaza hapo awali lilikuwa likitumia muda kufanya hivyo. Lakini kwasasa linajiwasha na kujizima within 5 to 6 minutes
Huyu jamaa ana mawengee tuu
 
Friji langu aina ya Boss linawaka na kuzima. Ukiwasha linafanya kazi kwa dakika takribani mbili Kisha linazima kwa dakika kadhaa, halafu linajiwasha tena. Hivyo ndugu zangu waliowahi kukutana na changamoto hii naombeni msaada tafadhali?
Tatizo ni umeme hapo current inayoflow hapo haipo stable ndio maana fridge guard inatedect na kukata.
 
Friji langu aina ya Boss linawaka na kuzima. Ukiwasha linafanya kazi kwa dakika takribani mbili Kisha linazima kwa dakika kadhaa, halafu linajiwasha tena. Hivyo ndugu zangu waliowahi kukutana na changamoto hii naombeni msaada tafadhali?
Umecheck temperature setting ipo ngapi? Ni kawida, ubaridi ulioweka ukigikiwa inazima. zukitaka iwake almost continuously, weka the minimum temperature
 
Itafute hio thermostat kwenye friji uitoe then problem solved

Kunakua na thermometer ikifika ubarid flani friji linajizima automatic niliwahi kutana na hio case nilichofanya niliivuta thermometer nikaiweka nje ya friji habari ikaisha
 
Unamponza mwenzio. Hiyo ni friji na sio gari.
 
Awali lilikuwa linafanya hivyo ila si kwa kuwaka na kuzima kwa dakika chache. Lilikuwa linatumia muda mrefu kidogo, linawaka kwa zaidi ya saa kisha linazima kwa dakika kadhaa. Lakini sasa hivi linafanya hivyo ndani ya dakika 5 tu kujiwasha na kuzima hali ambayo siyo ya kawaida kabisa.
Kaangalie sehem ya kuseti ubaridi kuna mtu amechezea. Mi kuna dogo aliweka no6 fridge ikawa inawaka non stop ikawa inachapa umeme balaa. Nuja kustuka kumbe dogo alipandisha ubaridi hadi mwisho. Nikarudisha recomended ambayo ni 4 sijaona shida, so angalia pengine kuna mtu kaseti0 ama 1
 
Ni kweli mkuu nilitatua hii shida kwa utaratibu uliosema. Ilifika kipindi Nikaona nimepigwa dukani huko, kumbe ni setting tu za friji
 
Back
Top Bottom