mangikule
JF-Expert Member
- Jun 11, 2012
- 6,369
- 5,866
Hivi kuna anayemsifia bwana joni mwendazake! Kuna mtu anataka kulinganisha butiama na chato? Mkuranga na chato? Lupaso na chato? msoga na chato?Kiukweli nilitokea kumchukia sana hayati Magufuli hasa kwa mambo 'binafsi' hata kabla hajawa rais!
Ila pamoja na yote Magufuli alikua ana afadhali ukimlinganisha na Kikwete au Samia tuongee tu kwa kumtendea haki.
Ni nani hakupapendelea kwao nchi hii?
Nyerere na Mara? Nyerere na akina Butiku?
Mwinyi na Zanzibar/Mkuranga?
Mkapa na kusini?
JK?
Pili kuna haja gani ya kutumia rasilimali kubwa hivyo kuchapisha kitabu chenye maudhui yasiyo na msaada? Lengo ni kujifunza? Kama ni kujifunza si tunayo historia ya Gbadolite huko Zaire sasa DRC? Nani ana fadhili hayo na kwa maslahi gani?
Magufuli ni lost case kwa sasa haya hayatusaidii.
Mwisho tuwe makini sana na waandishi uchwara maana huu ni ulaji unatafutwa kwa mtu na ni njia ya kututoa kwenye reli.
tuwe tu serious jamani! watanzania hatuna umakini wowote kwenye uchaguzi wa viongozi!
Huyu aliyeuza nyumba za serikali binafsi akiwa waziri na kugawia michepuko yake?
Huyu aliyediriki kuchepusha barabara ipitie nyumbani kwake chato akiwa waziri?
Tukubali kujifunza kwa maandiko haya tusije kujisahau tena
Tukachagua U4- Uthubutu - Ushupavu - Ubinafsi - Ukabila. Tuwachunguze watu tunaowapeleka ikulu!
Tulipigwa kiboko baada ya kutojali ule ubinafsi aliouonyesha akiwa waziri.
Nilikuwepo kwenye mojawapo ya kampeni zake sehemu ya biharamulo ambao aliwanyima barabara iliyokuwa ipitie kwao! walipomlalamikia aliwaambia hivi- "kunyeni mavi mubandike barabarani iwe lami"
Huko Kigamboni aliwaambiaje kuhusu kushusha bei ya nauli ya pantoni? "kama hamna hiyo hela pigeni mbizi"
Lugha za uhuni/ukibaka na akathibitisha kwenye uongozi wake kwa kutuwekea mavibaka kama kina Sabaya, Makonda nk.
Ansbert andikeni kitabu kingine kuhusu umuhimu wa hekima katika uongozi.