From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

Yaliyojificha uwekezaji wa Hayati Dk Magufuli Chato yawekwa vitabuni​

Ijumaa, Aprili 14, 2023
magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.

Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.

Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.

Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.

Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.

Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.

"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Mwamba Bado yu hai hajafa ndo maana anatisha watawala na wahuni wote bajeti kwa ajili yake ipo na itakuwepo maana Bado yupo hai
 
Huo ni upambavu wa kiwango cha SGR na kuna mtu kawalipa.Waongee lingine, kwenye suala la miradi hapo wamechemka!
Reli ya SGR inaenda Chato?Mradi wa Umeme Rufiji upo Chato?Bandari kavu ya Kwala ipo Chato?Mradi Ujenzi wa mji Mkuu wa serikali upo Chato?Ujenzi wa vituo vya Afya zaidi ya 300 vipo Chato?Kijazi Flyover ipo Chato?Mfugale Flyover ipo Chato?Barabara ya njia nne Kimara mpaka Kibaha ipo Chato?
Kwa uchache,Waandishi wameongozwa na chuki zaidi ya uhalisia.
JK mwenyewe alipeleka umeme Kijiji cha Hoyoyo, Mkuranga ambapo hakuna mradi wowote bali Umeme alipata Mkwewe Baba yake na Salma na shambani kwa mkewe!
Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ambao alizindua mwaka 2014!
Inshort Kibanda na Ngurumo kama wamo humu jukwaani wajue wamejidharirisha akiwemo na Baba Askofu!.Ila Ngurumo nadhani stress za kukimbia nchi zinamsumbua!
Umekisoma kitabu? Au unajibu hoja usiyoijua?
 
Nimefurahi sana kusikia kitabu kimeandikwa kuhusu mtu mwovu Magufuri.

Nafikiri kama vita vya wenyewe Kwa wenyewe vitatokea basi kaburi lake tutaenda kulilipua kama kulipiza kisasi kwa watu walioonewa kipindi chake.

Alikuwa mwovu fedhuri sana

Aendelee kuungua motoni na aongezewe moto.

Mungu tutaendelea kukushukuru kwa tendo kuu la kumuua huyo mwovu. Leo nchi yetu ingekuwa na wakimbizi kibao.
 
..hakuna haja ya kufurumusha matusi.

..watetezi wa Magufuli nao waandike kitabu.

..waandishi wote waliokuwa wakimsifu na kumpamba Magufuli wakati akiwa hai wako wapi?

..Musiba, Kabudi, Makonda, etc wanasubiri nini kunyanyua kalamu zao kuandika kuhusu Magufuli?
Kila watu waandike kitabu chao.

Maisha yako ndio kitabu chako.
 
Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.
Hakika jiwe alikuwa dikteta!
 
Yaliyojificha uwekezaji wa Hayati Dk Magufuli Chato yawekwa vitabuni​

Ijumaa, Aprili 14, 2023
magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.

Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.

Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.

Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.

Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.

Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.

"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Sadness, twende na Samia
 
Back
Top Bottom