FT: 2022 Uefa Champions League Final | Liverpool 0-1 Real Madrid | Paris, France

FT: 2022 Uefa Champions League Final | Liverpool 0-1 Real Madrid | Paris, France

Habari zenu mabibi na mabwana!

Leo ni sikukuu kubwa barani Ulaya na Duniani kwa ujumla. Ni mchezo wa Fainali ya Uefa Champions League kati ya Liverpool Vs Real Madrid.

Awali fainali hii ilipangwa ifanyike jijini Saint Petersburg, nchini Urusi. Ila kutokana na Urusi kuivamia Ukraine Uefa wakahamisha fainali hiyo jijini Paris nchini Ufaransa.

Hii itakuwa fainali ya tatu kuzikutanisha timu hizi mbili, ambapo mara ya kwanza walikutana mwaka 1981 hapahapa jijini Paris na Liverpool kubeba ndoo hiyo kwa 1-0.

Fainali ya pili kuzikutanisha timu hizi ni mwaka 2018 kule jijini Kiev ambapi Madrid alishinda kwa mabao 3-1 shukrani za pekee zilimuendea Sergio Ramos kwa kumtengua bega Mo Salah.

Kwahiyo hii itakuwa Fainali ya kisasi baina ya timu hizo mbili. Huku mashabiki wakisubiria kwa hamu mtanange huo.

Uwanja huu wa Stade de France, umewahi kuandaa fainali mbili tangu uanzishwe ile ya mwaka 2000 ambapo Real Madrid alitwaa kombe kwa kumfunga Valencia. Na mara ya pili kwa uwanja huu kuandaa mchezo wa fainali ya UCL ni pale Barca alipotwaa ubingwa dhidi ya Arsenal mwaka 2006. Kwahyo tuseme uwanja huu unazibeba sana timu za Spain.

Liverpool wataingia katika mchezo huu wakitafuta ubingwa wao wa 7 wa UCL baada ya kuzitoa timu kama Inter Milan, Benfica na Villareal, wengi wakisema Liverpool alipitia njia nyepesi.

Real Madrid watashuka dimbani kutafuta ubingwa wao wa 14 wa UCL baada ya kuzitoa timu ngumu kama PSG, Chelsea na Man City na wengi wakisema wamepitia njia ngumu.

Refarii wa mchezo huu ni Clement Turpin kutoka nchini Ufaransa. Mwamuzi huyu mwaka 2021 alichezesha Fainali ya Europa League kati ya Villareal Vs Man Utd ambapo Villareal walitwaa ubingwa kwa mikwaju ya penati. Mwamuzi huyu ana miaka 40 hivyo atalimudu vyema pambano hilo.

Mchezo huu utapigwa majira ya saa 4:00 Usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki na utakuwa live kupitia Dstv chaneli namba 223 kifurushi cha Compact. Bila kusahau Canal nao watakuwa mubashara.

Tukutane hapa kwa updates huku mimi nikiwapa nafasi Real Madrid kutwaa ndoo! Karibuni sana...
Mimi siipendi Madrid Ila ni Bora wakachukua kuliko Liverpool,
Hatutalala jamani, hatutalala.
 
Huku YANGA huku Liverpool [emoji91][emoji91][emoji91]
20220228_220236.jpg
 
Madrid lazima tumuangushie mtu mninga
 
Liverpool ataingia kwenye hii match akiwa amekamia (kutaka kulipa kisasi) , asichojua ni kwamba Madrid anaweza akaamua ushindi wake hata kwenye injury time, ili game angalau iwe competitive basi clopp aanze na hawa watu

Mane, Diaz, jota

Kiungo

Henderson, Fabio, keita

Ukuta wa nyuma

Trent, matip, Robertson,vvd

Kipa

Allison


Napo kipigo kipo pale pale, sana sana watapunguza idadi ya magoli
Poleni sana
 
Back
Top Bottom