Soka hamuliwezi, ila mkiambiwa muwekeze kwenye michezo mnayoiweza mnakaza fuvu. Mataifa yenye akili yalishatambua yana vipaji gani na ndo walikowekeza, hawahangaiki na soka wasiloliweza.
1.Kenya, Ethiopia na Jamaika - Riadha
2.USA na sasa South Sudan - Basketball
3.South Africa na India - Cricket
Tanzania mnashindwa nini kuwekeza kwenye Boxing ambako mnatisha Afrika yote? Mbona Rashid Matumla na wenzake walishawaletea mikanda mingi ya Africa ila kwenye soka hamjawahi kuleta kombe kubwa? Shida yenu ni nini?