FT: Al Ahly 1-1 Simba SC (Agg, 3-3)| Africa Football League| Simba yaondolewa kwa Goli la Ugenini

FT: Al Ahly 1-1 Simba SC (Agg, 3-3)| Africa Football League| Simba yaondolewa kwa Goli la Ugenini

Hawa al ahly nao Sijui wamekuaje siku hizi
Wamekutana na moto
68e43208-0548-41b3-b9e7-83d50e9c8a5b.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bocco hakabi wala hana uwezo wa kukaa na mpira, sijui kocha alifikiria nini kuanza na Bocco ilhali mpira anaocheza leo ni wa kutumia counter attack. Kwa aina hii ya mchezo unawezaje kumtegemea Bocco ambaye hata kutuliza mpira ni kazi kwake.?


Pale South Africa Mamelod wamegoma kumuachia kipa wao namba moja wa zamani (Onyango) licha ya kuwa hachezi, nadhani ni kwasababu wanampenda sana ndiomaana analipwa mshahara akiwa benchi. Kama Simba Sc wanampenda sana Bocco, ni vyema wakamlipa mshahara akiwa benchi badala ya kulazisha vitu ambavyo haviwezekani tena.


Utashangaa Bocco anarudi uwanjani.
Niliwaza kumuanzisha Bocco ili Baleke awe plan B au angeanza Phiri napenda sn Baleke akiingia sub km wakipatikana Baleke mwingine simba itakua nzuri sn Bocco mwakani wampe majukumu mengine
 
Mnatoka ikibaki hivi hivi
Acha tutoke maana haitakuwa sawa na ambaye hakuingia kabisa.

Tutatoka tukiwa tumeionesha dunia mpira wa Tanzania jinsi tulivyo u-inspire.

Tutatoka tukiwa tume wave flag ya Taifa na kuthibitisha kuwa haikuwa makosa kufanya uzinduzi kwenye ardhi ya Tanzania huku mwakilishi akiwa ni Simba.

Tutatoka tukiwa tumeacha alama ambayo itadumu milele na haijikufutika kuwa Simba ambao kikosi chao hakizidi thamani ya 7 Bilioni kilimpeleka putaputa Al Ahly ambaye mchezaji wake mmoja alisajiliwa kwa 12 Bilion.

Tutatoka tukiwa tumeiachia Dunia maswli mengi kwanini Club namba moja Duniani kwa mataji mengi leo hii ikutane na upinzani mkali hivi tena katika ardhi ya nyumbani?

Baada ya hayo yote ndio itapopatikana sababu ya Tanzania kuwa mwenyeji na mfunguzi wa AFCON.
 
Back
Top Bottom