Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Bayern Munich Vs PSG; Leo! leo! leo! kazi ipo Ubavu chuma upande mwanaume mashine
Bayern Munich, wakiwa nyumbani katika dimba la Allianz Arena mbele ya mashabiki wao, wanawakaribisha Paris Saint-Germain kwenye mkondo wa pili wa nusu fainali ya UEFA Champions League. Mchezo huu utapigwa saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Katika mkondo wa kwanza uliochezwa kwenye dimba la Parc des Princes, PSG walitumia vyema uwanja wao wa nyumbani kuibana Bayern kwa ushindi wa mabao 5-4 katika mchezo uliokuwa wa kasi na ushambulizi wa pande zote.
Mshindi wa jumla katika dimba hili atasonga mbele kucheza fainali dhidi ya Arsenal tarehe 30 Mei 2026 kwenye uwanja wa Puskás Aréna, Budapest, Hungary, baada ya Arsenal jana (5 Mei) kutumia vyema uwanja wa nyumbani kuifunga Atlético Madrid kwa bao 1-0.
Nani atasonga mbele kuelekea fainali? ⏳⚽