FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ile game ngumu na ambayo inafuatiliwa kwa ukaribu sana na watu wote wapenda soccer la africa, game ya robo final ya caf champions league baina ya miamba kwelikweli, timu zenye misuli ya kutosha, Simba sports club vs Wydad athletic club. Ni palepale machinjioni ambapo yeyote akitia maguu pale, hutoka vichwa chini miguu juu.

Hakika mnyama anaitaka hii mechi na hayupo tayari kuona anagota robo final pekee.

Wachezaji mahiri wa mnyama wote watakuwepo kutupa raha watz wote na bila shaka leo kila mtu ataishabikia
simba sports club.
Wanalunyasi.
Taifa kubwa.
Samba loketo.
Mwana kulitaka.
Mwana kulipata.
Wazee wa kidedea.

Timu iliyobarikiwa na MUNGU na inayosakata kabumbu lililothibitishwa na caf na kufurahiwa vilivyo na fifa mpaka kupelekea sikukuu ya eid icheleweshwe hapa nchini kwetu pekee ili kuingoja mechi hii ya kibabe.

Nikuanzia saa 10:00 jioni, tuwe wote mwanzo mpaka mwisho kwa updates zote.

Eid mubarakh
Tambo zoote hizi mkuu, kumsifia huyu Simba wa tong'areng.... Halafu shangaa simba anapakatwa! Wala sitashangaa....

Maana wana simba soka linachezwa mdomoni! Na Sio uwanjani!....
 
Freekick tunaoata hapa dakika ya 3 ya mchezo
 
Aisee ile pasi chonganishi ni very risk
 
Back
Top Bottom