FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Kabla ya mechi wachambuzi wa mchongo walisema simba anakufa Goli 5, baada ya mechi wasema ni kawaida Wydad ni kawaida kufungwa akiwa ugenini

Haujawaelewa wachambuzi yaani goli 5 ukijumrisha na mechi ya marudiano mwarabu kwake anakufa 4 Na hili la leo yanakua magoli 5
 
Reference angalia game zote za UEFA hatua ya robo fainali..Timu zote zilizopata matokeo game za kwanza ndio hizohizo zilizofuzu... i.e Manchester city,inter,AC milan and real Madrid
 
Simba Vs Al Ismailia, 2-0 ikasimamishwa na iliporejewa 1-0
Hii mechi inanikumbusha mtoto wa ki zanzibar mmoja wa kuitwa shehan rashid, yaani watu walifuta maji kwenye pitch ili penalt ipigwe. Dah waarabu walipoona maji ya shingo mechi ikapelekwa kirumba kama sikosei
 
Reference angalia game zote za UEFA hatua ya robo fainali..Timu zote zilizopata matokeo game za kwanza ndio hizohizo zilizofuzu... i.e Manchester city,inter,AC milan and real Madrid
Wee mawe, yani UEFA ufananisha na upupu wa Africa kweli zimo wewe?
 
Hongera kwa ushindi, na hasa goli zuri ambalo mchoro wake hakuna angeweza kuuchora kabla.

Nafasi ya Simba kufuzu ipo ikiwa itakuwa bora kimbinu kuwazidi hao Wydad Casablanca.

Wydad walianza kuvutavuta na kukamata wachezaji wa Simba. Ile ni ishara gani, kuzidiwa au mbinu za mchezo?

Chama apunguze zaidi mbwembwe, Kuna goli ilikuwa afunge leo.

Makocha na wachezaji watenge muda kurejea hii mechi katika video.

Ule mchezo wa away, wajipange kumiliki zaidi pale kati.

Kasi ya Wydad kule Morocco itakuwa mara dufu, ni kazi ya makocha kubuni mbinu.

Simba irejee video zote za mavurugu ya Morocco, iwe mvua, kelele, tarumbeta nk waone kawaida.

Ule mkakati wa kuitoa Zamaleki 2013 uboreshwe zaidi. Simba ioneshe haijafika hapa kwa kubahatisha.

Hakuna lisilo wezekana na Wala haitakuwa miujiza Simba kuingia nusu fainali.

Kuna watauliza kwa wachezaji gani? Ni hawahawa, mbinu na bidii zaidi Simba wanavuka kibabe.

Mengi yalisha fanywa na Simba huko nyuma, kwanini isiwezekane sasa.
Karibu [emoji1666] Casablanca Morocco kila goti litapigwa
182191-sports-football-club-afrique-maroc-wydad-athletic-club.gif
 
Back
Top Bottom