FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Azam Tv Max ni janga la kitaifa, najaribu kustream live hapa zbc 2 inaandika ujumbe huu " This content is restricted in your area "...

How ? Kivipi yaani? Kifurushi kipo active tangu wiki iliyopita cha 23k.. Nipo Tanzania bara..Au Azam Tv Max, chaneli za Znz ni kwa ajili ya upande wa pili tu..

Au ni mimi peke yangu nakumbana na hiyo changamoto ya kupata chaneli ya zbc 2 kwa app ya Azam tv max?

Au siku ya mechi kubwa huwa hawaiweki hewani kupitia App?
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ile game ngumu na ambayo inafuatiliwa kwa ukaribu sana na watu wote wapenda soccer la africa, game ya robo final ya caf champions league baina ya miamba kwelikweli, timu zenye misuli ya kutosha, Simba sports club vs Wydad athletic club. Ni palepale machinjioni ambapo yeyote akitia maguu pale, hutoka vichwa chini miguu juu.

Hakika mnyama anaitaka hii mechi na hayupo tayari kuona anagota robo final pekee.

Wachezaji mahiri wa mnyama wote watakuwepo kutupa raha watz wote na bila shaka leo kila mtu ataishabikia
simba sports club.
Wanalunyasi.
Taifa kubwa.
Samba loketo.
Mwana kulitaka.
Mwana kulipata.
Wazee wa kidedea.

Timu iliyobarikiwa na MUNGU na inayosakata kabumbu lililothibitishwa na caf na kufurahiwa vilivyo na fifa mpaka kupelekea sikukuu ya eid icheleweshwe hapa nchini kwetu pekee ili kuingoja mechi hii ya kibabe.

Nikuanzia saa 10:00 jioni, tuwe wote mwanzo mpaka mwisho kwa updates zote.

Eid mubarakh
Hapo mwamba ni wydad pekee maana ni bingwa mtetezi,ANAKOMBE,Simba umwamba katolea wapi Kwa kombe LIPI?
 
Azam Tv Max ni janga la kitaifa, najaribu kustream live hapa zbc 2 inaandika ujumbe huu " This content is restricted in your area "...

How ? Kivipi yaani? Kifurushi kipo active tangu wiki iliyopita cha 23k.. Nipo Tanzania bara..Au Azam Tv Max, chaneli za Znz ni kwa ajili ya upande wa pili tu..

Au ni mimi peke yangu nakumbana na hiyo changamoto ya kupata chaneli ya zbc 2 kwa app ya Azam tv max?

Au siku ya mechi kubwa huwa hawaiweki hewani kupitia App?
Ni kwa wengi sana mkuu ipo ivo. bora wewe imeandika is restricted in your area. Sisi wengine ukifika muda wa game za caf chaneli inapotea kabisa huioni hata kwenye list.

Wapuuzi sana aisee
 
Kikosi hiki mmmh
20230422_152144.jpg
 
Washenzi sana
Nilikuwaga nailipia online kwa azam max app. Ila ninamuda sana siilipii maana lengo langu lilikuwa ni kuona games za CAF tu.

Jaribu kudownload yaccine tv wanarusha game za CAF na zingine nyingi tuu. Huwa natumia hiyo app mimi.
Watarusha kupitia channel gani..hiyo app nnayo
 
Back
Top Bottom