FT: CAFCC FINAL 22/23 First Leg | Yanga SC 1-2 USM Alger | Mkapa Stadium | Mei 28, 2023

FT: CAFCC FINAL 22/23 First Leg | Yanga SC 1-2 USM Alger | Mkapa Stadium | Mei 28, 2023

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Leo ndio leo hatimaye imefika siku muhimu kwa wapenda soka barani Africa.

Ni fainali ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Africa kwa msimu wa 2022/2023 kati ya Yanga na USM Algerz Mechi hii itachezwa mnamo saa 10 jioni kwa saa za Africa mashariki kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Timu hizi katika historia zimeingia fainali kwa mara ya kwanza, na pia ziliwahi kukutana kwenye msimu wa 2018 ambapo Yanga alifungwa kwa hiyo mechi hii inaweza kuwa ya kisasi

Nini kitatokea?

Karibuni kwa live updates kuanzia mwanzo, kati na hata mwisho wa mtanange huu muhimu!

Kwa wanaofuatilia kwenye TV, Azam (ZBC 2) na DSTV ( Chaneli namba225) watarusha mubashara mechi hii.

===
Kikosi cha Yanga SC
IMG_7349.jpeg


Kikosi cha USM Alger
IMG_7350.jpeg

Mchezo umeanza
2' Mchezo umeanza kwa kasi kubwa, Yanga wanafika langoni kwa wapinzani
3' Tayari timu zote zimepata kona mojamoja
9' Hali ya uwanja ni mvua wachezaji wanateleza mara kwa mara
11' USM Alger wanatupia mpira wavuni lakini tayari mwamuzi anasema ni offside
15' Yanga wanakosa nafasi ya wazi, shuti la Tuisila linadakwa na kipa
18' Mchezo bado una presha kubwa, wanashambuliana kwa zamu
22' Mayele anakosa bao, mpira unapita nukta chache kutoka kwenye mstari wa lango
32' Goooooooooooooooooooo
Aimen Mahious anaipatia USM Alger goli kwa njia ya kichwa
39' Goli walilofungwa Yanga ni kama limewapunguza presha
45' Zinaongezwa dakika 3

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
46' Yanga wanapata faulo karibu na lango la wapinzani
Shuti kali la Azizi Ki linatoka nje
48' Oussama Chita anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Azizi Ki
50' USM Alger wanapata kona
58' Adem Alilet wa USM Alger anapata kadi ya njano
62' Yanga wanapata kona, inapigwa inaokolewa
66' Mchezo umesimama wachezaji wawili wa Alger wameumia
70' Yanga wanaendelea kupambana kutafuta goli la kusawazisha
81' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mayele anafunga goli zuri akimalizia pasi ya kichwa ya Mudathiri
83' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
USM Alger wanafunga goli la pili kupitia kwa Islam Merili
90' Zinaongezwa dakika 10

FULL TIME
 
Waarabu wanakuja kufanya dhihaka kwenye nchi ya kikapuku ya kilofa
 

Na kwakua mliwahi kusema mafanikio yenu yamechangiwa na kubezwa na mashabiki wa Simba.

Basi nasisi leo tutaangalia namna bora ya kuwafanya mpate motisha ya kuzidi kukaza, mchukue kombe.
 
Leo ndio leo hatimaye imefika siku muhimu kwa wapenda soka barani Africa

Ni fainali ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Africa kwa msimu wa 2022/2023 kati ya Yanga na USM Alger

Mechi hii itachezwa mnamo saa 10 jioni kwa saa za Africa mashariki kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Timu hizi katika historia zimeingia fainali kwa mara ya kwanza, na pia ziliwahi kukutana kwenye msimu wa 2018 ambapo Yanga alifungwa kwa hiyo mechi hii inaweza kuwa ya kisasi

Nini kitatokea?

Karibuni kwa live updates kuanzia mwanzo, kati na hata mwisho wa mtanange huu muhimu!

Kwa wanaofuatilia kwenye Tv.. Azam (zbc 2) na Dstv ( Chaneli namba225) watarusha mubashara mechi hii
Nami nakubali yanga leo atashinda zaidi ya goli 3 mengine sijui
 
Utafikiri unakimbizwa!? Pumua kidogo basi.... Kwani kuanzisha uzi huwa mnalipwa!?
 
Kama mapema vile ! au tayari ?
samahani Mkuu , sikujua kama uko kwenye kamati ya ulinzi wa Uwanja
 
Back
Top Bottom