FT: CAFCC FINAL 22/23 Second Leg | USM Alger 0-1 Yanga SC 03/06/2023

FT: CAFCC FINAL 22/23 Second Leg | USM Alger 0-1 Yanga SC 03/06/2023

Medali bila komba ni sawa na zile shanga za kienyeji za kutibu tonsils, kule kwa wasukuma wanayaita MATUYUYU [emoji1].

Mimi usinieleze habari za michuano isiyoeleweka eti SHIRIKISHO, njoo kulw kiumeni tupambane ili ujue ukubwa wa hiyo robo unayoiponda hapa.
Shanga sisi hatuzijui labda wanapewa wanao ishiaga robo ndio maana wewe unazijua mpaka zinapopatikana, inawezekana mpaka sasa mnazo pair nne maana robo mmeishia mara nne. Sisi tunazo zijua medali na leo tumeziona live wachezaji wakivaa.

Hii michuano unayoiita haieleweki, ndio iliyokufanya ubebe lundo la kuni na vibiriti ukaota moto katikati ya uwanja na ukapigwa faini ya dola elfu kwa kuharibu pitch ya watu South.

Uzuri kaka yako Yanga kaenda kukufutia aibu baada ya kulitia aibu taifa.
 
Umepata nn msimu huu , hebu ongeza sauti kwanza [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Ngoja nikuweke wazi pengine hukupata bahati ya kusoma nilichokiandika kwenye uzi fulani.

Ni kwamba hivi

Mwaka jana kwenye kombe la dunia isingewezekana kwa mimi kufika hadi fainali kama ningekuwa nashabikia timu moja.

Kushabikia timu moja ni too risk unaweza ukakosa kila kitu.

Kwa kulijua hilo sasa nikuanbie tu, huko majuu nina kalabao nishaweka kabatini.

Hapa Afrika tayari leo nimepata kombe.

Kwa hiyo kukosa kwako wewe ubingwa dhidi ya USM ALGER hauwezi ukatumia hoja ya mimi kukosa ubingwa kama niia ya kujipatia furaha.

Na hii itawahitaji mchukue miaka 30 mingine mje mfike hatua kama hii.
 
Ifike hatua tuwe serious kama taifa gharama zilizotumiwa na serikali kwenye huu upupu tungekuwa na kituo cha afya kama si shule
 
Mkuu najua umetamani kusiwe na fainali ya home and away kwa sababu umeshinda mechi ya pili lakini haukuchukua kombe.
Ungeshinda Leo huko huko kwa idadi ya magoli ya kukuwezesha kuchukua kombe nadhani wala usingeandika ulichoandika.

Sasa hebu jiulize hivi, mechi ile ya kwanza kati ya yanga na usma iliyochezwa Dar ndo Ingekua mechi moja pekee na ya mwisho kwa matokeo yale,ungejisikiaje?
Kwa Mkapa ilikua Usma 2 - 1 Yanga.
Kwa matokeo hayo yange ndo ilishashindwa kuchukua kombe pia .

kama kusingekua na mechi ya pili nadhani ungetamani kuwe na mchezo wa marudiano.
Kumbuka hii mechi ya Leo ndio imekupa nafasi ya kufunga goli moja bila.
Hoja yangu ni huru sana sababu mm si uto ila nimewaheshimu kwa kufa kiume.

FAINALI MBILI HAINOGI MGENI ANAPOSHINDA. HATA KISAIKOLOJIA HAIJAKAA SAWA. INATAKIWA UWANJA NEUTRAL MASHABIKI 50/50
 
Zilikuwa timu 32, zikabaki 16, zikabaki 8, kisha 4, kisha 2... Bahati ikawa kwa USMA kuwa Bingwa, lakini Yanga itabaki kuwa timu bora
Hata kwenye darasa la wajinga, wakawanza na wa pili hupatikana.

Hatupaswi kuisifia Yanga kwa kuonekana nzuri miongoni mwa team za kijinga, kwanini hakuwa bora huku CAFCL?
 
Hakika historia imewekwa na Dunia nzima imeshuhudia na vizazi vinavyokuja vitakuta haya mliyoyafanya WACHEZAJI wote wa YANGA SC.

PONGEZI sana tena sana.

Nia tunayo, Naamini mshikamano huu ukiendelea basi hii itakuwa TIMU tishio AFRIKA.

Ahsanteni YANGA.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
timu tishio wapi ww? Umemuona nabi akilia lakini?
 
Sheria za kijinga sana hizi ndo maana wenzetu waliondoa huu upuuzi.
Fainali iwe moja tu.
Africa aisee imekaa kipigaji sana aisee
Kama fainali Ingekua moja yanga bado wanheshindwa kuchukua kombe.
Maana walishafungwa 2 kwa 1 nyumbani kwao.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unakuta Kuna kijanaume nacho kinasimama kinashangilia USMA kuchukua kombe huku kimelowa kimoko 😅😅, afu ukikiuliza haya USM amechukua vipi wewe una nini kwenye kabatini ni tobo tu.
 
Back
Top Bottom