Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
- Thread starter
- #141
Kwani hakuna watu waliosema Simba atakufa 8 kwa Wydad?Huo mpira wanaocheza USM ndio mpira mpya kwao wameanza kuucheza kwenye mechi ya leo? Inawezekana vipi Marumo aweze kumfunga goli mbili kwa sifuri kwa huo mpira wao halafu Yanga washindwe?
Yanga mpaka anafika hapa kakutana na timu tofauti tofauti ngapi? Kumbuka kuna watu + wachambuzi + mashabiki walisema Yanga atakufa mengi kwa Madiba kutokana na aina ya mpira wa Marumo kuwa wana kasi, wana uwezo wa kumiliki mpira, wanapiga pasi na wako compacted na wana intensity lakini nini kimetokea leo?
Mpira ni mbinu, unaingia na approach kulingana na mpinzani wako unayekutana nae.
Sioni sababu ya Yanga kushidwa kumfunga USM, ikiwa hao Marumo wameweza kumfunga magoli huyo mwarabu magoli mawili. Sio mpira wa kutishana bali ni mpira wa kujipanga. Yanga ilipofikia hapo kaishacheza na timu zenye mpira tofauti tofauti kwanzia kwa Al Hilal, Club African, Monastir, Real Bamako, Tp Mazembe, Rivers hadi kwa Marumo. Kocha akija na mbinu nzuri anawafunga kama walivyofungwa wengine tu
Hao watu hamkuwahi kuwaita hater au wanaichukia Simba kwasababu ni timu ambayo hamuipendi.
Acheni unafiki sometimes