Ni kweli mkuu hata Real Madrid wenye makombe 14 ya UCL, walipigwa 4-0 na Manchester City ambao walikuwa hawana kombe hata moja la UCL, ila huwezi kusikia watu wanasema Real Madrid ni timu mbovu kisa hilo
Lakini bongo kuna watu wanakuambia eti Simba ni timu mbovu kisa imepigwa 5-1 mara moja tu na Yanga, tena wakijua kabisa kwamba golini alikaa kipa ambaye ametoka kwenye majeraha, na hajadaka kwa muda mrefu sana
Anyway acha tusubiri tarehe 1/12, ndugu zetu watakapokutana na Al Ahly ndipo wataujua uwezo halisi wa timu yao, hawa ndugu zetu kwao hiyo sentensi ya "mpira hautabiriki" huwa hawaielewi