Leo ndo leo majira ya saa 4 usiku Yanga sc watakuwa wanacheza mechi yao ya kwanza katika ligi ya mabingwa Afrika Mungu ibariki Yanga SC.
YANGA YAANZA VIBAYA MAKUNDI CAF, YAPIGWA 3-0 UGENINI
Ikicheza kwenye Uwanja wa Stade du 5 Juillet Nchini Algeria, Yanga imeshindwa kutamba baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-0 dhidi ya CRBelouizdad katika mchezo wa Kundi D kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF)
Magoli yamewekwa wavuni na Abdelraouf Benguit (10), Abderrahmane Meziane (45) na Lamin Jallow (90)
Mchezo ujao, Yanga itaikaribisha AlAhly ya Misri kwenye Uwanja wa Mkapa, Desemba 2, 2023