FT: England 2-1 D.R. Congo | World Cup 2026 | Mercedes-Benz Stadium | Julai 1, 2026 | 1:00 Usiku

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
England wanatarajia kuonyesha kiwango bora zaidi wanapoanza hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia 2026, wakisafiri hadi jijini Atlanta kukabiliana na DR Congo katika mchezo wa hatua ya 32 bora.

Licha ya kumaliza vinara wa Kundi L kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Panama katika mchezo wa mwisho wa makundi, England hawakuwavutia mashabiki wengi kwa kiwango walichoonyesha katika hatua hiyo. Hali hiyo imeongeza presha kwa kikosi hicho kinacholenga kufika angalau robo fainali kwa mashindano makubwa ya tano mfululizo.

Kwa upande wa DR Congo, huu ni wakati wa kihistoria kwani watacheza kwa mara ya kwanza kabisa hatua ya mtoano katika Kombe la Dunia. Walifanikiwa kufuzu baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika Kundi K, huku ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uzbekistan ukiwasaidia kuwa miongoni mwa timu bora zilizomaliza nafasi ya tatu na hivyo kupata tiketi ya hatua inayofuata.

Historia ya Mikutano

England na DR Congo hazijawahi kukutana katika mechi yoyote ya kimataifa. Hata hivyo, hii itakuwa mara ya tatu kwa England kucheza dhidi ya timu kutoka Afrika katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, ambapo walishinda mechi zote mbili zilizopita dhidi ya wapinzani kutoka bara hilo.
 
Mleta mada amelala
 
Hakuna cha kuangalia sifa za kwenye makaratasi! Acha dk 90 ziongee!! Uingereza ulimi nje!!
 
Watu weusi ni bure kabisa, hiimechi ilitakiwa iwe japo 0 - 2 half time. england wanafunguka sana, hawa DRC kule mbele kuna watu wenye nguvu na kasi lakini waliokosa akili na maarifa
 
DRC wanazingua sana.
 
England wafanye mpango wa Saka ili wazidi kuichosha defence ya Kongo. Kumbuka ikichoka tu zinaingiakama maji. Congo abadilishe kiungo aingie mwenye nguvu zaidi nankasi zaidi Moutassau na Sadiq wanatakiwa kuongezea nguvu au watolewe washatepeta.
 
Ila huyu kocha DRC kwa nini hampi nafasi Mayele!! Zile kosa kosa kwa Mayele muda huu tungekuwa tunaongea mengine!!
Nafasi ya ubora duniani Uingereza ni ya 4 wakati DRC ni ya 46!! Hayo ni makaratasi! lakini hali halisi ndani ya uwanja mpaka mapumziko: DRC 1 0 UINGEREZA!
Swali je ule ushamba wetu wa Afrika wa kuanza kusinzia dakika za majeruhi na leo utajirudia? Harry Kane wasimchukulie poa kama Ivory Coast walivyomchukulia poa Halaand! Alichowafanyia dk za majeruhi hawatakisahau!
 
Back
Top Bottom