FT: England 2-1 D.R. Congo | World Cup 2026 | Mercedes-Benz Stadium | Julai 1, 2026 | 1:00 Usiku

FT: England 2-1 D.R. Congo | World Cup 2026 | Mercedes-Benz Stadium | Julai 1, 2026 | 1:00 Usiku

Kuna Jamaa wa Serbia bado nazidi kuamini maneno Yake kuna mdau alibisha humu, ni kwamba wachezaji wa kiafrika Ikifika dakika ya kuanzia sitini basi wanapoteza concentration, wanaanza kufanya maamuzi ya kijinga jinga yasiyo na maana...

Hili nahisi lipo kwenye damu, muda wa tukio unapozidi kwenda basi umakini unaanza kupungua, je Hili sio kweli hata kwenye maisha yetu?...
Sasa zikifika dakika hizo si ndio zipigwe sub zote 5 ili wachezaji wapya waingie na concentration ya kushinda!
 
Mbona Ufaransa wengi ni Waafrika na wanacheza vizuri tu? Kuna wakati wazawa huwa watatu tu.
Ufaransa kwenye soka, wanamaanisha biashara, hawana masikhara. Hawaoni shida kabisa kuwa na timu yote yenye wachezaji weusi. TFF wanashindwa kabisa kutoa wachezaji 20 leo wenye umri wa miaka 10 wakawapeleka academy tofauti za timu ukubwa ulaya, wakajifunza soka kwa miaka 7, wakirudi hapa tunakuwa na kikosi cha hatari. Wao kazi kujadili mambo ya Simba na Yanga na ccm
 
Hao wapya wanaongia wanajua sio waafrica au?

Umeeambiwa Wachezaji wa kiafrica inamana haijalishi ameanza mechi au ameanzia benchi
Sasa zikifika dakika hizo si ndio zipigwe sub zote 5 ili wachezaji wapya waingie na concentration ya kushinda!
 
Tatizo ni mental concentration!! DRC na ENG hawakupishana sana footwork. Lakini mental & physical stamina DRC kazidiwa kwa mbali sana na ENG!
 
Lazima tukubali kwamba baada ya wazungu kugundukua Wao ni copy ya Africa basi wakajiletea football ili kujifariji, bahati mbaya tukashobokea na sisi mwisho wa siku tunaonekana ni copy mbaya ya wazungu
 
Hao wapya wanaongia wanajua sio waafrica au?

Umeeambiwa Wachezaji wa kiafrica inamana haijalishi ameanza mechi au ameanzia benchi
Basi hili ni tatizo kubwa sana. Mtu hata hajaingia uwanjani lakini anaingia na kupoteza concentration. Tunawahitaji sana wazungu kusogea hapa
 
Back
Top Bottom