FT: Kaizer Chiefs 4-0 Simba SC | Klabu Bingwa Afrika CAFCL | FNB Stadium

🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Simba kama timu leo tumezidiwa kwa mbinu,jamaa wametuzidi na wametufunga,pasi chache wapo golini wanatukisa nyavu.
Pana mtu kasema game plan yenu haikuwa nzuri nadhani nakubaliana nae kwa kuwachezesha Mkude na Lwanga na Bwalya kwangu naona haikuwa sawa. Yote kwa yote poleni watani tizameni makosa yenu bado pana mchezo mmoja
 
Unataka kukimbilia wapi ww kujaaaa
ushaliwa weye....
 
Umeandika kiushabiki zaidi,Simba inawachezaji bora,kufungwa leo goli nne haijalisha kuwa Simba sio bora.
Kwenye mpira kuzidiwa na kufungwa ni kawaida kwenye soka.
Simba nguvu moja.
Mchezaji bora nani? Ukiona mchezaji anakuja kucheza ligi ya bongo ujue huyo ni galasa. Tanzania hatuna hela ya kununua wachezaji bora. Mtu akipata zero form four, ukimpa mtihani wa la saba lazima aonekane kipanga
 
Pana mtu kasema game plan yenu haikuwa nzuri nadhani nakubaliana nae kwa kuwachezesha mkude na lwanga na bwalya kwangu naona haikuwa sawa. Yote kwa yote poleni watani tizameni makosa yenu bado pana mchezo mmoja
Hakuna cha game plan mkuu leo Simba imezidiwa kwa mbinu chache sana tena sana.
Kaizer hawakua na mambo mengi na kila nafasi waliyopata walitumia vema kwa 90% kupata magoli.
Simba ni timu hasa tena ni timu bora ila kwenye soka kufungwa kupo na hauwezi kushinda ama ku-draw kila mechi lazima kuna siku utafungwa tena kwenye hatua muhimu ya kusonga mbele kama hatau ya leo kwa Simba.
 
Hata tukiwapiga nne tutaenda kwenye matuta.
Mkuu mpaka mnawapiga hizo nne wao wanakuwa wamesinzia?

Kosa kubwa mlilolifanya Simba leo ni kuruhusu goli nne zote! Maana yake mna kibarua kigumu sana cha kurudisha hayo magoli
 
Mchezaji bora nani? Ukiona mchezaji anakuja kucheza ligi ya bongo ujue huyo ni galasa. Tanzania hatuna hela ya kununua wachezaji bora. Mtu akipata zero form four, ukimpa mtihani wa la saba lazima aonekane kipanga
Simba ni bora na ina wachezaji bora ndo maana imefika robo wakiongoza kundi la kifo kundi"A" na upambanaje wake mpaka kufika robo umeonekana wazi na kila mtu ameona.

Kwenye soka kuna matokeo matatu, Simba ni timu bora.

Sisi kama mashabiki wa Simba tuna imani na timu yetu na haya ya leo ni sehemu ya soka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…