FT: Kaizer Chiefs 4-0 Simba SC | Klabu Bingwa Afrika CAFCL | FNB Stadium

FT: Kaizer Chiefs 4-0 Simba SC | Klabu Bingwa Afrika CAFCL | FNB Stadium

Timu mbili kutoka Nchi marafiki, Afrika Kusini na Tanzania zinakutana leo Jumamosi ya Mei 15, 2021 kwenye uwanja wa kwanza Afrika kuchezwa fainali za Kombe la Dunia, ambapo Kaizer Chiefs wanakabiliana na Simba SC katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa FNB Stadium nchini Afrika Kusini.

Mchezo inatarajiwa kuwa mkali na wa vuta nikuvute kwa muda wote wa dakika 90, mchezo ambao utachezwa bila kuwepo mashabiki uwanjani.

Kaizer Chiefs wakiwa nyumbani katika hatua ya makundi hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye uwanja wa FNB, wameshinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja huku wakiwa hawajaruhusu bao kwenye michezo yote mitatu.

Simba SC ushindi wa michezo minne na sare ya mchezo mmoja huku ikiwa wamepoteza mchezo mmoja na kujikusanyia alama 13 na kumaliza vinara wa kundi A wanakipiga na Kaizer Chiefs wakiwa wameshika nafasi ya pili kwenye kundi C kwa alama 9.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 kwa saa za Tanzania na saa 12:00 kwa saa za Afrika Kusini.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.

Kaizer Chiefs Vs Simba SC

===============

00' Mpira umeanza dimba la FNB

04' Almanusura Kaizer waandike goli la kwanza baada ya Manya kubaki na goli lakini akajigonga, kona.

05' Goooooooooaaal Kaizer Chiefs wanatangulia kwa bao la kwanza, mpira ulioanzia kwenye kona. Kaizer Chiefs 1-0 Simba SC

11' Chris Mugalu ansshindwa kuipatia Simba SC bao, baada kushindwa kumalizika pasi ya Miquissone

Simba wametulia sasa wanacheza kwa kupasiana kujaribu kupenya ngome ya Kaizer Chiefs.
Safi sana
 
Tulieni mpira uchanganye vizuri, asitoke Kapombe akianza kuwakimbiza hao wasauzi ndio watamjua vizuri.
 
afadhari mnanitia myo kwa kuonyesha namna Simba anavyopiga kandanda huko.
 
Simba hakwenda sauzi kushambulia, kaenda kukaa na mpira apoteze muda, kama goli likitokea ni bahati sio mbaya, ila primary objective kucheza away ni defence.
 
Yule beki gani wa Simba alitaka kutoa boko,badala ya kuucheza mpira yeye anataka kutumia mwili na mwili wenyewe hana,tena ndani ya penati box?
 
Back
Top Bottom