FT: Namungo FC 0-2 Yanga, Ligi Kuu, Uwanja wa Majaliwa (Lindi), 07/12/2022

FT: Namungo FC 0-2 Yanga, Ligi Kuu, Uwanja wa Majaliwa (Lindi), 07/12/2022

Namungo badala ya kucheza kwa kuwaheshimu Yanga wanacheza kwa kuwaogopa! Wanacheza huwezi kuamini ni wachezaji wa ligi kuu! Very poor performance! Unfortunately kocha wao mkuu ndio kocha wa Taifa Stars? Shame!
Hivi ihefu watacheza lini tena na yanga kelele zipungue huuku mtaani? Maana Namungo wametuangusha

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Namungo badala ya kucheza kwa kuwaheshimu Yanga wanacheza kwa kuwaogopa! Wanacheza huwezi kuamini ni wachezaji wa ligi kuu! Very poor performance! Unfortunately kocha wao mkuu ndio kocha wa Taifa Stars? Shame!
Ukitazama vizuri utaona kwamba kuna baadhi ya mechi Yanga huwa inashinda si kwamba siku hiyo wanakuwa Bora ILA timu wanayocheza nayo inakua hivyo hovyooo ........mchezaji hata akili ya mpira inakua ndogo .....quality ndogo , nafasi nyingi za wazi wanapoteza .......

Angalia mechi ya prison na nafasi walizopata prison ...namungo, Kagera sugar....
 
90' Mwamuzi anamaliza mchezo
90' Zinaongezwa dakika 4 za nyongeza
85' Yanga wanaendelea kufanya mashambulizi
Tuisila Kisinda anafunga goli la pili kwa Yanga
82' GOOOOOOOOOOO
75' Namungo FC wamepata nafasi kadhaa za kupiga mashuti langoni kwa Yanga
66' Bado mambo ni magumu kwa Namungo, wapo nyuma kwa bao 1-0
59' Kasi ya mchezo inaongezeka
55' Yanga wanatengeneza mipango kwa kupiga pasi nyingi
50' Bado mchezo ni wa ushindani, wanapeana zamu kushambuliana
Kipindi cha pili kinaanza

MAPUMZIKO

45' Namungo wanapambana kusawazisha
Yannick Bangala anafunga baada ya kipa wa Namungo kuutema mpira
GOOOOOOOOOOOOO
40' Yanga wanapata faulo
35' Presha ya Yanga inaongezeka
26' Namungo wanafika langoni mwa Yanga lakini wanakosa umakini
20' Mayele anaonekana kuwa chini kama mwenye maumivu
18' Mayele anaangushwa ndani ya boksi lakini mwamuzi anapeta
11' Yanga wanamiliki mpira muda mwingi
9' Fei Toto anapiga shuti linapaa juu ya lango
5' Kasi ya mchezo bado haijachanganya
Mchezo wa Ligi Kuu Bara, umeanza, Yanga wakiwa ugenini, wanakaribishwa na Namungo FC.

View attachment 2438847
Kikosi cha Yanga

View attachment 2438869
Kikosi cha Namungo FC

Yanga wamemrejesha mshambuliaji Fiston Mayele katika kikosini cha kwanza baada ya kukosekana mchezo uliopita, wakati Namungo wakifanya marekebisho machache ‘benchini’ akiwepo Pius Buswita.
Yanga baba lao
 
Mayele kaisha sana. Asiporudi Kongo kwenda kuchochea dawa sidhani kama ataweza kufunga goli Tena msimu huu
Mara nyingi mmesema hivyo. Wapo hata walimuendea kwa songoma. Wakatangaza kabisa tayari tumeshika miguu. Alivyotupia tena kwa kasi wakaambiwa wamekosea masharti kwa sangoma
 
Yanga mmeshinda against timu iliyocheza ovyo mno! Leo hatujaona ubora wa Yanga zaidi ya Namungo mbovu!!
Kama ilivyokuwa ngao ya hisani nayo ilikuwa hivyo hivyo na timu yenu ya kumtegemea mchezaji mmoja.
 
Ukitazama vizuri utaona kwamba kuna baadhi ya mechi Yanga huwa inashinda si kwamba siku hiyo wanakuwa Bora ILA timu wanayocheza nayo inakua hivyo hovyooo ........mchezaji hata akili ya mpira inakua ndogo .....quality ndogo , nafasi nyingi za wazi wanapoteza .......

Angalia mechi ya prison na nafasi walizopata prison ...namungo, Kagera sugar....
Msimu Yanga mechi aliyo cheza hovyo ni moja tu na Kagera Sugar.Unaizungumzia timu hiyo ya juzi iliyo Park bus mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom