FT: Namungo FC 0-2 Young African SC | NBC Premier League | Majaliwa Stadium | 30.11.2024

FT: Namungo FC 0-2 Young African SC | NBC Premier League | Majaliwa Stadium | 30.11.2024

Mimi nalaumu sana kwanini timu zimeanza kuwafunga yanga mapema hivi, ilitakiwa zianze kuwafunga baada ya dirisha dogo ili wasijue madhaifu yao wakija kushituka wamekosa ubingwa, hata hii mechi ya leo naombea washinde tu ili wajipe moyo ubora wao umerudi wasihangaike kusajili tena
 
Watu huwa wanaanzisha uzi wa mechi siku moja kabla ila toka YAS (Yanga Atafungwa Saaaana) ianze rasmi kwa vipigo vitatu mfululizo, leo kumekuwa na kigugumizi katika kuanzisha uzi wakati yamebaki masaa machache mechi ianze.

Vyura mmesusia timu yenu? Tunaomba msijidhuru tu maana vipigo vinaendelea kama kawaida.

Binafsi nadhani mnaenda kufungwa mechi 6 mfululizo ndiyo kuna katimu mtakaotea baada ya hapo.
Uzi ulikuwepo mbona
 
Mimi nalaumu sana kwanini timu zimeanza kuwafunga yanga mapema hivi, ilitakiwa zianze kuwafunga baada ya dirisha dogo ili wasijue madhaifu yao wakija kushituka wamekosa ubingwa, hata hii mechi ya leo naombea washinde tu ili wajipe moyo ubora wao umerudi wasihangaike kusajili tena
🤣🤣🤣
Umeshaona tunashinda sio
 
Leo mtajua haya mambo mawili
1. Khomeiny ni bonge la goalkeeper
2. Musonda ni bonge la striker!
 
Sikuwa mfuatiliaji kabisa wa mechi za Yanga ila hapa karibuni wameanza kunivutia kuwafuatilia. Hebu kipute kianze tupate rubudani.
 
Sijui kuhusu matokeo ya mwisho ila naamini Mpumelelo anaendelea pale alipoishia

Mechi ya juzi Afisa Habari wenu aliwaambia mje mmevaa kamba kiunoni, msivyokuwa na adabu wengine mkaja na shanga.

Mechi imeisha watu wanakuja kufanya usafi kwa ajili ya mechi ya kesho wanakuta getini kumejaa makolokolo ya ajabu, mikamba mikamba, mishanga.

Sijajua na mechi ya leo kama kutakuwa na muendelezo wa kampeni "tutafungua vilivyofungwa"
Mpumulelo ameanzia benchi bana 🤣
 
Huyu kocha anapewa maelekezo. Licha ya malalamiko ya watu kwamba Aziz ki amechoka, bado kampanga na chama yuko nje.
 
Sikuwa mfuatiliaji kabisa wa mechi za Yanga ila hapa karibuni wameanza kunivutia kuwafuatilia. Hebu kipute kianze tupate rubudani.
Muendelee kulia pamoja 🤣🤣
 
Back
Top Bottom