Leo mnamo majira ya saa 3 usiku Klabu ya Tanzania Simba Sports Club itakuwa nyumbani kumenyana na klabu ya Al Ahly ya Misri katika mechi ya mkondo wa kwanza (First Leg) wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Maandalizi ya timu zote mbili yameenda vyema, kinachosubiriwa ni mchezo rasmi leo 29/03/2024 saa tatu usiku.
Ungana nami katika uzi huu ili kupata matukio mbalimbali yatakayojiri kabla na wakati wa mchezo huo.
Karibu.
==============
Timu ya Simba inatarajia kucheza dhidi ya Al Ahly ya Misri katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, leo Machi 29, 2024
Takwimu zinaonesha hakuna mbabe mpaka sasa, kila upande umeshinda mechi Tatu, hizi ni mechi zilizopita baina ya timu hizo:
24/10/2023 Al-Ahly 1-1 Simba
20/10/2023 Simba 2-2 Egypt
09/04/2021 Al-Ahly 1-0 Simba
23/02/2021 Simba 1-0 Al-Ahly
12/02/2019 Simba 1-0 Al-Ahly
02/02/2019 Al-Ahly 5-0 Simba
29/08/1985 Al-Ahly 2-0 Simba
22/08/1985 Simba 2-1 Al-Ahly