FT: Simba 2-0 Yanga | NBC PL | Benjamin Mkapa Stadium | 16.04.2023

FT: Simba 2-0 Yanga | NBC PL | Benjamin Mkapa Stadium | 16.04.2023

Yanga wameangushwa na beki mbovu ambao walionekana kuwa na kiwewe toka dakika ya kwanza na kuacha mianya ambayo Simba walitumia ipasavyo pia Mayele alitakiwa aondolewe kipindi cha pili baada ya kuumia.
 
Yanga kuna weakness mahala, haiwezekani, kuna hujuma ndani kwa ndani, kikao cha dharura haraka sana, hujuma zote ziangaliwe, kama kuna mchezaji au wachezaji wamehongwa au referee au hujuma yoyote lazima uongozi iangalie upya haraka
[emoji16][emoji16][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Hivyo ndivyo zilivyo mechi za watani wa jadi, zinamalizwa nje ya uwanja maana ata wachezaji wa Simba baada ya mechi ukiwauliza walishinda vipi mechi ambayo kipindi Cha pili unashambuliwa muda wote hawatakua na jibu.
Hongera Kwa mbumbumbu fc mganga wao kafanya kazi kubwa sana.
 
Mechi ya leo imeamulia na saikolojia ya wachezaji, nyuso za wachezaji wa Simba walikuwa na shauku kubwa sana ya kudhihirisha kitu mbele ya wapenzi wa mpira wa miguu ulimwenguni kutokana na kukosolewa kwao kuwa ni kikosi kibovu huku Yanga kwavile wanaongoza ligi na hawajapoteza moja tu wakiaminika kuwa ni bora zaidi. Hali ya kujiamini na kuchukulia mazoea ikaingia kwa mashabiki, wachezaji hadi benchi la ufundi.

Simba walijiandaa sana kiakili kwa hali ya juu hivyo ikawa ni rahisi kwa kuwa ndani ya mchezo katika game plan yao. Yanga kipindi chote cha kwanza walipoteana kabisa, akili zao zilikuwa hazijatulia, halafu wakawa wana mambo mengi mno uwanjani wakati wachezaji wa Simba walikuwa ni kwenda direct na kwa haraka golini kwa Yanga. Kutokana na kuwa na utulivu makosa kwa wacheza wa Simba yakawa ni machache kulinganisha na Yanga waliopotea mchezoni. Kilichowakuta leo ni kama surprise, na yote hiyo ni kutokana na kutokuheshimu mpinzani wako.

Kama hii mentality itabadilika, basi kule kwa Rivers Yanga itapigwa goli nyingi sana. Maana saivi kila mtu anamuonea Simba huruma huku wakijiona wao wapo semi, ila mambo yanaweza kwenda tofauti.

Mwisho namalizia kwa kusema, Yanga msimu ujao ubingwa wa NBC mnapaswa mjipange sana. Ukiangalia kikosi cha Simba kinahitaji tu kiungo mkabaji basi. Ila Yanga inahtaji wapishi wa magoli haswa na namba tisa ambaye asubiri nafasi kumi ndio apate goli moja.
Pia soma hapa namna nilivyompa tahadhari mwana yanga mwenzangu kuamini Simba ni mbovu.

 
Hatimae YANGA imekipata kilichomnyoa Paka Manyoa.Kelele nyingi eti HAMFUNGIKI nyinyi nani hata MSIFUNGIKE? Hatimae leo ndani ya DIMBA la MKAPA Mmechinjwa HADHARANI bila HURUMA.Tumekuwa tunawaambia Kwa mujibu wa REKODI za CAF Klabu ya SIMBA ni Klabu zaidi yenu licha ya nyinyi kuongoza Ligi.
Ushahidi mwingine YANGA ndio Mabingwa wa Ligi lakini mmeshindwa kuendelea na Michuano ya Mabingwa mkaangukia Michuano ya WASHINDWA na SIMBA ambao sio Mabingwa Wanacheza KOMBE la MABINGWA.HONGERA sana Klabu ya SIMBA kwa USHINDI MTAMU na Kuifanya DUNIA NZIMA IFURAHI.
Hatimae SIMBA 2
YANGA 0
 
Yanga wameangushwa na beki mbovu ambao walionekana kuwa na kiwewe toka dakika ya kwanza na kuacha mianya ambayo Simba walitumia ipasavyo pia Mayele alitakiwa aondolewe kipindi cha pili baada ya kuumia.

Kwa kawaida mipira ya adhabu au fouls za namna hiyo mtu mmoja au hata wawili wanapaswa kumzonga mtu anaetaka kuanzisha Ili kupata nafasi ya kukaa kwenye position za kuwabana wapinzani. Sasa wao foul inatokea mtu anaanzisha haraka hakuna wa kumchallenge au hata wengine kuwa makini kwa wamiliki wa mpira Ili wasiruhusu wanabaki kushangaa tu. Sijui kwanini timu hazijifunzi kwenye mipira ya namna hii
 
Nabi ana matatizo makubwa kwenye ufundishaji wake. System yake ikifeli haina mbadala. Huu uchezaji wa pass nyingi na nyingi zikiwa ni back pass hauna maana, huwa anacheza kama mchezo ni siku nzima. Simba waneizidi Yanga kwenye mambo mawili tu, precision na aggression.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Makolokolo Vs Wydad Casablanca kwanza tujue tuna kikosi bora au tulikamia tu mechi ili ubingwa wa Yanga - NBC PL 2023 usitangaziwe mikononi mwetu.
 
Back
Top Bottom