SIMBA AMKENI…
Nawakumbusha tu mafanikio ya Mpira ni mataji na sio pesa wala kujaza uwanja.
Kiuhalisia mmekubali kuendeshwa na hili sakata la ujazaji wa Uwanja na badala ya kuhoji ni msimu wa ngapi huu mnajaza huo Uwanja lakini hamna mataji?!
Naona safari hii ndio Uongozi umezidi kuwahadaa kwa kuwaletea Mgeni Rasmi ambae ni namba Moja hapa Nchini, hivyo kuwasahaulisha kuhoji maswali ni je lini mtarudi kwenye zama za kunyanyua makwapa?!
Wenzenu wana Siku ya Mwananchi ambayo inaambatana na kuwaonesha washabiki wao kile walichovuna msimu uliopita, yaani Mataji, sasa Je Simba mnawaonesha nini Washabiki wenu?!
Washabiki wa Simba hizi sherehe za Siku moja zisibadili mfumo wa ufahamu vichwani mwenu na kuwafanya mkose akili ya kuhoji mambo ya maana na haswa hili suala la timu kushindwa kufanya vizuri kwa zaidi ya msimu wa 3 sasa.
Well Simba Day imefana.
Haya kuanzia Kesho tuwahoji Viongozi kwanini Timu inashindwa kubeba Mataji na kila kitu inapata?!
Hojini, hojini, hojini…
Waulizeni Viongozi wenu ni lini mtarudi kwenye zama zenu za kutesa na Simba Day huku mkitambulisha mataji?!
Wakishindwa kutoa majibu ya kueleweka basi wapeni muda na wakishindwa kurudisha hadhi ya Simba ile ya Mataji basi wawajibike.
Amkeni wana Simba, Viongozi wenu wanawatumia kama Kopo la Chooni, yaani wanawatumia wakiwa na shida zao tu miongoni mwao ni kuficha madhaifu yao kwa hili Tamasha la Simba Day, na zikiisha wanawaacha kulekule Chooni.