FT: Simba Day | Simba SC 2-0 Power Dynamos | Benjamin Mkapa | Agosti 6, 2023

FT: Simba Day | Simba SC 2-0 Power Dynamos | Benjamin Mkapa | Agosti 6, 2023

Utimamu wa mwili SIMBA bado sana...
Cjui kama wana mazoezi ya nguvu.
Nimeona Onana, Ngoma , Kibu, micquson wakipushiwa tu wanahama njia...
Fanyieni kazi haraka kama lakini mna mawazo ya SUPER LEAGUE..
TULITEGEMEA MPIRA wa kasi, pasi za haraka haraka wakifungua vyumba ...Badala take angalau nimeona hilo kwa Dynamo..
Wenyeji umetubeba...

Cjui labda tusubiri
Leo utahaha sana,tangu mwanzo wa tamasha mpaka sasa umehangaika sana kukosoa na hujafanikiwa.Tamasha la Simba Day limekutesa sana siku ya leo.
 
Wanasemaga akili ni nywele kila mtu anazake, ila hawaja identity za eneo gani.Kama kwa utashi wako unaona ni sawa basi it's ok.
Na pia siyo lazima kile serikali ya kichwa chako inavyokitafsri ndicho kiwe sahihi,mwingine anaweza kuangalia hilo tukio kwa angle tofauti na akaja na tafsiri yake pia na akawa sahihi pia
 
Na pia siyo lazima kile serikali ya kichwa chako inavyokitafsri ndicho kiwe sahihi,mwingine anaweza kuangalia hilo tukio kwa angle tofauti na akaja na tafsiri yake pia na akawa sahihi pia
Kila mmoja akawa na tafsiri yake, ila still bado haiondoi ubaya wa hiko kitu.

Mfano tohara serikali inasema ni mbaya,ila ukienda huko Manyara,Singida, Kondoa kwao tohara ni sahihi,so kuona sahihi kwao bado hauondoi ubaya wa tohara
 
Wamechukua albino na kumvalisha pampas,then alichokuwa akikifanya kwenye jukwaa kwa maelekezo ya maMC ni kitu kikichoshusha utu wake.Siajajua kama na yy kweli ni mzima kiakili au anauchizi fulani.

Mpira ni mchezo wa wastaarab,waungwana na watu wenye heshima. Moja ya lengo la mpira ni kuwaunganisha watu na si kuwabagua wala kuwatenganisha, hichi kilicho fanyika leo,kama walizani kina mgusa Manara basi wamekosea sana kwani huu ni ubaguzi na unyanyasaji zidi ya albino kwani.
Kwahiyo Tanzania nzima albino ni manara tu?
 
Angefanya mtu mwenye ngozi ya kawaida ungelibeba hivi? Ni wangapi hufanya matukio ya hivyo kwenye matamasha haya, kwanini huyu Albino ndio iwe deal?

Yule ni mtu kama wewe na ana uwezo wa kufanya alitakalo, kwanini uhisi kuwa alitumwa, mbona wale weusi huwa hamsemi hivi?

WEWE NI MBAGUZI, tusio wabaguzi tunaona ni hali ya kawaida tu.

Wale ni watu watu kama wewe, wanachohitajini kutambulika na kuthaminiwa, sio HURUMA ZA KINAFIKI.
 
Simba Sc hatuna kocha, kwa style hii sitashangaa kuona wachezaji waliokuwa tishio kugeuka magarasa.

Kipaji cha Phiri kinaozea benchi bila sababu ya msingi, Kramo, na wageni wengine wote ukiondoa Malone na Onana, nao tutawaita magarasa msimu ujao.

Hii Simba Sc akipewa Mgunda anafika nayo mbali kuliko huyu jamaa, team ina talents nyingi ila hajui kuzitumia.

Tutarajie kikosi KAUKA NIKUVAE.
 
Angefanya mtu mwenye ngozi ya kawaida ungelibeba hivi? Ni wangapi hufanya matukio ya hivyo kwenye matamasha haya, kwanini huyu Albino ndio iwe deal?

Yule ni mtu kama wewe na ana uwezo wa kufanya alitakalo, kwanini uhisi kuwa alitumwa, mbona wale weusi huwa hamsemi hivi?

WEWE NI MBAGUZI, tusio wabaguzi tunaona ni hali ya kawaida tu.

Wale ni watu watu kama wewe, wanachohitajini kutambulika na kuthaminiwa, sio HURUMA ZA KINAFIKI.
Kweli akili ni nywele japo hawa kusema za eneo gani. Okay basi sawa.
 
SIMBA AMKENI…

Nawakumbusha tu mafanikio ya Mpira ni mataji na sio pesa wala kujaza uwanja.

Kiuhalisia mmekubali kuendeshwa na hili sakata la ujazaji wa Uwanja na badala ya kuhoji ni msimu wa ngapi huu mnajaza huo Uwanja lakini hamna mataji?!

Naona safari hii ndio Uongozi umezidi kuwahadaa kwa kuwaletea Mgeni Rasmi ambae ni namba Moja hapa Nchini, hivyo kuwasahaulisha kuhoji maswali ni je lini mtarudi kwenye zama za kunyanyua makwapa?!

Wenzenu wana Siku ya Mwananchi ambayo inaambatana na kuwaonesha washabiki wao kile walichovuna msimu uliopita, yaani Mataji, sasa Je Simba mnawaonesha nini Washabiki wenu?!

Washabiki wa Simba hizi sherehe za Siku moja zisibadili mfumo wa ufahamu vichwani mwenu na kuwafanya mkose akili ya kuhoji mambo ya maana na haswa hili suala la timu kushindwa kufanya vizuri kwa zaidi ya msimu wa 3 sasa.

Well Simba Day imefana.
Haya kuanzia Kesho tuwahoji Viongozi kwanini Timu inashindwa kubeba Mataji na kila kitu inapata?!

Hojini, hojini, hojini…
Waulizeni Viongozi wenu ni lini mtarudi kwenye zama zenu za kutesa na Simba Day huku mkitambulisha mataji?!

Wakishindwa kutoa majibu ya kueleweka basi wapeni muda na wakishindwa kurudisha hadhi ya Simba ile ya Mataji basi wawajibike.

Amkeni wana Simba, Viongozi wenu wanawatumia kama Kopo la Chooni, yaani wanawatumia wakiwa na shida zao tu miongoni mwao ni kuficha madhaifu yao kwa hili Tamasha la Simba Day, na zikiisha wanawaacha kulekule Chooni.
 
Wamechukua albino na kumvalisha pampas,then alichokuwa akikifanya kwenye jukwaa kwa maelekezo ya maMC ni kitu kikichoshusha utu wake.Siajajua kama na yy kweli ni mzima kiakili au anauchizi fulani.

Mpira ni mchezo wa wastaarab,waungwana na watu wenye heshima. Moja ya lengo la mpira ni kuwaunganisha watu na si kuwabagua wala kuwatenganisha, hichi kilicho fanyika leo,kama walizani kina mgusa Manara basi wamekosea sana kwani huu ni ubaguzi na unyanyasaji zidi ya albino kwani.
Kama wewe kimekugusa basi yeye kitamuuma sana japo siungi mkono tukio hilo.
 
Back
Top Bottom