FT: Simba Day | Simba SC 2-0 Power Dynamos | Benjamin Mkapa | Agosti 6, 2023

Ikiuma chomoa
 
Hongera nyie wenye malengo makubwa ya kufika makundi CAF champions league!! Yaani mkifika makundi mtafanya sherehe ya kufikia malengo mliyoyakosa miaka nenda rudi!! Ni halali yenu kuanzia mchangani!! Msione wivu!! Simba haianzii mchangani na malengo yake ni kufika nusu fainali champions league!!
 

UNYAMA UNYAMANI

Ukiangalia hizi Picha unaweza kuona Uhalisia uliokuwepo jana hii ndio maana kamili ya neno FULL HOUSE.

Mambo muhimu na ya msingi sana ambao wengine hawayataki kusikia ni kuwa Ilitangazwa siku Tatu kabla ya siku hii Tiketi zote zilikwisha SOLD OUT ila Ilitangazwa kuwa Mageti yatakuwa Wazi Kuanzia saa 2 asubuhi, ilipofika saa 4 asubuhi tayari kwa mujibu wa system ya NCard watu 16,000 walikuwa wameingia Uwanjani, ilipofika saa 6 mchana Watu 37,000 walikuwa tayari ndani ya Uwanja, ilipofika saa Saba na Nusu mchana watu 58,000 walikuwa wamekwisha ingia Uwanjani mwisho ni saa NANE NA NUSU Mageti Yote yalifungwa sababu Uwanja ulishajaa kupita kiasi na kwa mujibu wa Taratibu za Protocol zilitaka Kabla ya Mhe. Rais hajafika nje pawe salama na asiwepo mtu wa kuingia ndani tena Wanasimba waliwasaidia Watu wa Protocol kufanya hili masaa 2 kabla ya ratiba yao kufunga milango wao wakawa FULL HOUSE, sasa kama ulikuwa una tiketi ulikuwa unataka kuingia Uwanjani kilichokufanya usiingie ni kutofuata Taratibu za siku husika tunasema Pole sana lakini utakiwa umefurahia ulipo.

Hii ni Tukio ambalo limeonyesha ukubwa wa Simba CAF kutojuta kuiweka Simba katika African Super League na kutoa zawadi ya kutengeneza PITCH ya Mkapa Stadium kwa udhamini wa mashabiki wa Simba.

NYAMA ZIPO JUU KABISA KATIKA MTORI
 
watalipinga hili ila huo ndio ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…