Makocha inawezekana kabisa wana matatizo lakini most of the time tunawaonea bure, mkuu mimi ni simba kabisa lakini angalia jinsi kikosi chetu kilivyo dhaifu, naweza kusema ukitoa kile kikosi cha kwanza ambacho kinaanza kila siku kule benchi hakuna mchezaji ambaye utasema akiingia ataleta matokeo chanya kama timu ikiwaimefungwa au kuzidiwa, remember mechi ya juzi na Singida..., Kikosi ni finyu sana, kocha anakosa options, chama na okra walikosekana juzi singida, unaona kabisa hakuna mbadala wao.
Shida ya Simba inaanzia kwa Management
Hao ndo wakulaumiwa kwanza
Barbra, Try Again, Magungu
Hao watu 3 ndo wakubeba lawama.
Kupitia wao ndo tuna kikosi dhaifu, kikosi dhaifu ila kinachoitia timu hasara.
Simba walianzisha mambo ya kutoa 20mil kwa kila mechi, jambo ambalo sio sawa maana wale wachezaji kazi yao ni kucheza na kushinda mechi na si vinginevyo.
Simba imekuwa ikisajili kupitia mtu kuifunga au kupiga chenga nyingi.
Simba yaonekana haina scouts wazuri au mawakala wanaiibia. Mf Banda haifai Simba, ila sababu alikuwa mkopo Ulaya, mawakala wakaamua wapiga simba, nina uhakika Banda analipwa pesa nyingi sana kuliko aoneshacho uwanjani.
Kumuongezea Bocco mkataba wa miaka 2 ilikiwa kosa kubwa sana.
Kuelekea January
Bocco, Banda, Nyoni, Mkude, Kakolanya, Akpan, Okwa, Mwinuke, Gadiel, Kibu, Kyombo
Hawa waondolewe wachezaji wa maana waletwe, ikiwezekana kuvunja benki na kuvamia wachezaji wa timu za Azam.
Wamekuwa wakiwaondoa Makocha wakuu ila wanamuacha mtu mbaya Matola.
Ili Simba iendelee inabidi Management au Benchi la Ufundi na wachezaji waondolewe
Mikataba mipya ya wachezaji iwekwe kipengele cha kutofuzu makundi mishahara inapungua vinginevyo mchezaji avunje mkataba mwenyewe.
Mchezaji asipoperfom vizuri mshahara wake utapunguzwa