FT: Simba SC 1-5 Young African SC | NBC Premier League| Benjamin Mkapa Stadium | 05.11.2023

Sema mpira raha sana, kuna Yanga mwenzangu alikuwa kiti cha nyuma yangu, wakati tunashangilia goli la tano alipigwa konzi, mpaka mpira unaisha hajajua kapigwa na nani [emoji28][emoji28][emoji28]
Mie ningeangaliaga kwa watu wengi ningewamwagia maji kabisa,

Maana mnakelele balaa.

Kuna li bonge hapa jirani linafosi mabishano,

Wacha nilale zangu mie,

Nipeni pole na hela.
 
Suuukaaaaaaaaaaaaa simbaaaaaaa nguvu moya πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£pacomeeee
 
Poleni wanasimba. Ndo mpira huo. Mtatufunga safari nyingine. Na raha ya ushabiki ni kucheka na kufurahi. Kila la heri japo khamsa dah! Too much πŸƒπŸΏβ€β™‚οΈπŸƒπŸΏβ€β™‚οΈπŸƒπŸΏβ€β™‚οΈπŸƒπŸΏβ€β™‚οΈ

 
watu wameanza kumlaumu manula, yale magoli kipa yeyote alikuwa anafungwa. angalia kama kile kichwa cha musonda cha awali kabisa, kipa gani angedaka kile? angalia maxi alivyofunga, angalia aziz ki alivyopiga mpira kwenye miguu ya mabeki, angalia penati, magoli 4 yalikuwa ya kiwango cha juu, labda moja tu ndio pengine kipa bora angedaka.
 
Mie ningeangaliaga kwa watu wengi ningewamwagia maji kabisa,

Maana mnakelele balaa.

Kuna li bonge hapa jirani linafosi mabishano,

Wacha nilale zangu mie,

Nipeni pole na hela.
Sasa kwanini utumwagie maji sasa? πŸ˜…πŸ˜…

Anyways, pitia kwa wakala aliyepo karibu na home kwako hapo, nimekutumia hela ya pole mtani.
 
Sasa kwanini utumwagie maji sasa? [emoji28][emoji28]

Anyways, pitia kwa wakala aliyepo karibu na home kwako hapo, nimekutumia hela ya pole mtani.
Sipendagi makelele bana,nyie mnamakelele hadi kero.
 
Mkuu, nilianza kuipenda Yanga mwaka 2000 nikiwa katoto kadogo kabisa, wala huyu babe sikujua kama yupo duniani wala sikuwa najua kama kuna kitu mapenzi.
Mpira uko damuni, naupenda na kuujua haswa.
 
Try again, Mangungu na menejiment yote Simba Sasa nyumba inavuja Kazi kwenu!

Watu wa mpira , mashabiki na wapenzi wamesema sana, mkaweka pamba masikioni!

Wengine walidiriki kusema kwamba nyinyi sio watu wa mpira, mko Simba kwa masirahi yenu binafsi, kichaka chenu ni robo fainali na kumi bora Africa Kila mwaka! Sasa tunaanza kuamini, msimu wa tatu huu hamueleweki malengo yenu Nini!

Kawaida timu yenye mipango mizuri angalau iwe mtiririko wa

mafanikio, msimu huu robo, msimu ujao robo, msimu mwingine nusu, Sasa Kila msimu robo, Kuna shida mahala!

Sasa mtu wa mpira injinia Hersi anakuja kuwaumbua! timu yao inakwenda kwa mpangilio, na mtiririko mzuri wa kisoka.

Injinia ameshajua nini soka linahitaji , angalia scouting yake ya wachezaji, mwangalie max, mwangalie Yao , mwangalie Baka, mwangalie Azizi
Alafu njoo uwangalie na kina Onana Ayoub , kapama, utaona watu wa usajili wa Simba wana shida, Kila mwaka wanasajili na kuacha!
Ameondoka Mayele, Ameondoka Shabani, Feisali, Bangala na timu imezidi kuwa imara. Injinia tumpe maua yake!
Leo Simba tunatatizo la Kipa, lakini Cha kushangaza viongozi walikubali kumuacha kipa namba mbili Kakolanya wakati wakijua Aishi anaumwa na atakuwa nje muda mrefu, au ni kweli sio watu wa mpira!

Simba imesajili wachezaji wengi wa mbele imesahau Kuna kukaba pia, msimu karibu wa tatu huu hakuna kiungo mkabaji, timu inafunga usajili
Wala hawana habari na kiungo mkabaji, Ngoma sio mkabaji yule.
Mzamiru na kanute ni kwa sababu hatuna wachezaji imara, viwango vyao hafifu sana- mechi kama hizi ndio zinawaumbua Sasa!





Alafu tuache kusajili majina, tusajili vipaji. hawa kina Max hawakuja na majina, ni vipaji tu

Injinia angeakua anaangali majina, Leo hii Yanga tungewaona Kina. Yondani, Saidoo, Makambo Bado wanacheza- anajua mpira unahitaji Nini hawezi Fanya hivyo!


Alikuwa na mtu anaitwa Senzo, alivyoondoka akaletwa Mtine, unaweza usumuone umuhimu wake, kwa kuwa sio mtu wa media- lakini hawa ndio wapishi wenyewe!


Simba baada ya kuondoka Senzo- Kila kitu kwisha- Kuna haja ya kutafuta tena watu wa mpira kama hawa!
Upande wa makocha- huyu kocha wa mazoezi kutoka Rwanda atakuwa ana shida!
Ebu angalia kanute alivyoachwa na Paccone

Mgunda alitololewa bila sababu za msingi, kwenye Dunia ya mpira kocha anayefanya vizuri hatolewi, anayefanya vibaya ndio anatolewa, Robert amefundisha Rwanda, Kenya na Uganda, hakuna kikubwa amefanya, zaidi ya kumfunga Nabi akiwa na Viper, na nadhani viongozi wetu wakajaa kwa sababu hiyo!
Kipindi hicho Nabi alikuwa na unbeaten!
Injinia amemleta Nabi katusumbua, Gamondi anatusumbua, na atatusumbua sanaaa huyu injinia!

Angalau kipindi Cha kina Magori, Marehemu Hans pope, Mzee Rage, Manara , walituletea wachezaji wazuri!



Wachezaji hawana nguvu, mpira butua butua, timu haina muunganiko , sijui kama hata makundi kama tutatoboa

Huyu injinia, si muda mrefu analeta Kombe la club bingwa Africa!
Wanasimba, tutafute injinia wetu, hawa kina Magungu hawatatupeleka kokote, hawa wanasiasa tu!

Hongereni watani, ila viongozi Simba wanatuangusha sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…