FT: Simba SC 1-5 Young African SC | NBC Premier League| Benjamin Mkapa Stadium | 05.11.2023

FT: Simba SC 1-5 Young African SC | NBC Premier League| Benjamin Mkapa Stadium | 05.11.2023

Midomo yetu ni zege, leo tumefunga zipu
Tumekuwa legelege, tumemwagiwa upupu,
Acha tukapige mbege, kusahau hili kapu
Kama tulo na matege, tumepigwa chapuchapu

Natoa pongezi, kwenu leo mmepiga mwingi
Mmeweza toa dozi, kama mmepiga bangi
Mnaruka kama mbuzi, mmeshaingia kingi
Kweli mlienda kozi, muweze kuitwa Dingi
 
Back
Top Bottom