FT: Simba SC 2-2 Costal Union | NBC Premier League | KMC Complex | 4 Octoba, 2024

FT: Simba SC 2-2 Costal Union | NBC Premier League | KMC Complex | 4 Octoba, 2024

Kuwa mkweli Mtani yaani watu wanatokea nyuma na kuscore goli mbili halafu unasema sio mbaya.

Acha utani banaa. 😅
Mi nachokiona hapa wewe ndio unayetokea nyuma nyuma na kuanza kutunanga.

Mwanzo wakati uzi unaanza ulikuwa wapi?
 
Siamini yaani niliacha ubao 2-0 narudi nakuta Coastal wamefanya comeback ya ajabu. Shida ni nini wanasimba?

Pia tuzidi kuomba mechi ijayo uto nao watoe droo au wafungwe kabisa
Yanga ni masifa pro max kwenye derby lazima mnara wa 3G usome kwa Mbumbumbu fc otherwise hakikisheni Sasii ndie Pilato.

Mtani dua la kuku huwa halimpati mwewe.
Ila hapa kwenye dua tuna wasiwasi nasi pia wallah itabidi tuombe maana kimpira mbumbumbu hamtuwezi uto ila kwenye dua mnaweza kutushinda.
 
Ni matokeo mazuri kwa Simba , timu ilikuwa na madhaifu mengi ambayo yalikuwa hayaonekani sababu walikuwa wanapata ushindi.
Mpaka Sasa timu haina muunganiki Kila mchezaji anacheza anavyojua, kocha hawapi nafasi wachezaji wengine amekuwa ni mtu wa kukariri.
Kama watayachukulia kwa mtazamo chanya watasonga mbele Ila Kama watayachukulia kw mtazamo hasi itawakost.
yamekuwa haya tena?
 
Mbona kelele mingi..? Kumbe tumedroo tuu...
Tulieni jishikilieni vzr msitingishike...
Simba Bingwa....
Hii confidence huwa naizimia sana, mbumbumbu huruka nayo kuanzia mwanzo wa ligi hadi siku wanapokimbia kuvalishwa nishani za loosers third position!!

Kauli hizi huthibitisha kuwa Rage pekee ni genius simba nzima sababu ya kula sana asali ya nyuki wadogo kule kwao unyanyembe ruga ruga!!
 
Ha ha ha! Ni maombi tu, Tena wala huna haja ya kwenda kwa Mwamposa" unaweka vifungu, unapiga maombi!

Hawa Simba idadi yao ya magoli inatutesa, wanatakiwa kuondoka kwa point, wanaendelea vizuri, hili gap hawataliziba!
Simba haina tofauti na kagera sugar,
 
Leo ndo tunaangalia burudani sasa,
... maana Mechi ya jana ya Yanga ilikuwa ni zaidi ya maigizo yani haiwezekani Wachezaji wa Yanga wanakimbilia Golini kwa pamba wakafunge alafu wachezaji wa Pamba wanawafata huku wanatembea.

Pale ndo nikaelewa kwann yule Gabachori huwa anasema tu Yanga bingwa.
Haya
 
Back
Top Bottom