FT: Simba SC 3-1 Singida Fountain Gate | NBC Premier League | 12.03.2024

FT: Simba SC 3-1 Singida Fountain Gate | NBC Premier League | 12.03.2024

Nimeanza kuangalia mpira dakika ya 39.

Nilichokiona

Simba bado haichezi mpira wa kiushindani

Simba imejidhatiti sana kucheza mpira wa kiustaa.

Simba bado naiona imerudi kwenye utamaduni wake tuliokuwa tukiupiga vita wa kuridhika mapema pindi inapopata mabao ya kuongoza.

Big chance zinatengenezwa kila baada ya dakika 2 lakini hakuna goli linafungwa.

Mpira mpaka unaisha Simba itakuwa na big chances zaidi ya 10 lakini usikute magoli yakabaki hayo hayo 3 na pengine na clean sheets isiwepo.
 
Leo nimemtizama huyu bwana fredy koublan, nakiri ana sifa myingi za kuwa mchezaji mzuri, ana ball controll nzuri, dribbling nzuri, kupinga chenga(kumpita beki) anaweza.
Ila kinachomuharibu nahisi ni presha ama ndio alivyo ni mbinafsi, kuna vitu anafosi sana, kuna mipira ya kuachia ye anafosi, sehemu ya kupasia ye anataka kupiga, ubora wake hauwezi kuonekana kwa namna hii, walio karibu nae wampange. Kuna mpira mmoja alimchukua mtu vizuri ule ilibbidi ampasie saidoo kule pembeni, akaumg'ang'ania mpaka akapoteza, hata goli alilofunga, ilikuwa apasie.. Sasa hii kufosi anapokosea ndio inamuongezea presha zaidi, atashindwa kufamya vizuri kama mambo yakiwa yanamgomea hasa mabao.
 
Screenshot_20240301-210800_Google.jpg
 
Kingine naona simba bado hatuko na roho mbaya kwenye goli la mpinzani, tuna utoto mwingi, hii tabia hata kwenye champions league ilitugharimu game vs wydad hapa taifa.

Wenzetu UTOPOLO hawacheki na kima wakiwa golini.
Golini kwa mpinzani unahitaji uwe na roho mbaaaya sana.
 
Huyu kibu D graph yake inashuka.
Najiuliza aliyesema akili ni nywele ni nani, maana kibu nywele nyingi ila akili kisoda.
 
Tushamkanda 4
Hahaha yani nimegundua timu nikiwa na wasiwasi nayo ndio tunawakanda ila nikiwa nawadharau ndio wanatukanda, kama ile mechi na prisons iliniuma sana maana nilikuwa najiamini kuwa tutawakanda (siyo kwamba nilibet) maana wale hawatukamiagi sana, hawa singida nilikuwa na wasiwasi nao maana wao na azam wanatukamiaga sana ila nimeshangaa hadi sasa tushawakanda tatu basi mpaka hapa huu ushindi ni wetu
 
Back
Top Bottom