FT: Simba SC 3-1 Singida Fountain Gate | NBC Premier League | 12.03.2024

FT: Simba SC 3-1 Singida Fountain Gate | NBC Premier League | 12.03.2024

Leo nimemtizama huyu bwana fredy koublan, nakiri ana sifa myingi za kuwa mchezaji mzuri, ana ball controll nzuri, dribbling nzuri, kupinga chenga(kumpita beki) anaweza.
Ila kinachomuharibu nahisi ni presha ama ndio alivyo ni mbinafsi, kuna vitu anafosi sana, kuna mipira ya kuachia ye anafosi, sehemu ya kupasia ye anataka kupiga, ubora wake hauwezi kuonekana kwa namna hii, walio karibu nae wampange. Kuna mpira mmoja alimchukua mtu vizuri ule ilibbidi ampasie saidoo kule pembeni, akaumg'ang'ania mpaka akapoteza, hata goli alilofunga, ilikuwa apasie.. Sasa hii kufosi anapokosea ndio inamuongezea presha zaidi, atashindwa kufamya vizuri kama mambo yakiwa yanamgomea hasa mabao.
Sio yeye tu, wachezaji wa Simba wana hili tatizo la kulazimisha sehemu isiyofaa kulazimisha kisha mpira unapotea. Anafanya sana Saidoo, Kibu, Onana, Chama japo si mara nyingi, Sasa hivi kaongezeka Fredi.
 
Kingine naona simba bado hatuko na roho mbaya kwenye goli la mpinzani, tuna utoto mwingi, hii tabia hata kwenye champions league ilitugharimu game vs wydad hapa taifa.

Wenzetu UTOPOLO hawacheki na kima wakiwa golini.
Golini kwa mpinzani unahitaji uwe na roho mbaaaya sana.
Kwakweli bado tunaleta ujamaa kwa wapinzani kwa kuwaonea huruma, inatakiwa tukifika golini tuoneshe ubepari wa hali ya juu, tuna tabia ya kuridhika mapema
 
Saidoo kapiga upande aliopo kipa na wakati kuna upande upo wazi. Wanamchosha Chama, anafanya kazi kubwa halafu wakumalizia wanakosa.
Simba yetu ni mbovu ila hii singinda ni team mbovu kabsa
 
Sio yeye tu, wachezaji wa Simba wana hili tatizo la kulazimisha sehemu isiyofaa kulazimisha kisha mpira unapotea. Anafanya sana Saidoo, Kibu, Onana, Chama japo si mara nyingi, Sasa hivi kaongezeka Fredi.
Uko sahihi, wanafosi, mwishowe wanaharibu, inawahatibu kisaikolojia. Mwishowe wanajikuta wanachukiwa na mashabiki.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Hakuna mpira wa kufunga kila nafasi...
Alhaly mashindano ya club bingwa group stage kaongoza kwa kukosa clear chances ndo ije kuwa Simba?
 
Duuh ila na ww mbona unawasema sana wachezaji?
Mimi sinaga ushabiki maandazi, mbona simsemi ngoma, tshabalala na wengine, ukweli ni kwamba ngoma na baadhi ya wachezaji wanazingua kwa mazimgira tofauti, kibu nguvu nyingi akili kisoda
 
Wakati nyinyi mnahangaika kulinganisha chama na pacome,
Usikute siku simba anacheza, pacome anakaa na daftari lake kukopi notes kwa chama anaeishia ishia. [emoji1787][emoji23]
Mkuu watu wanaleta ligi tu ila kuna clip niliiona instagram ila sikuidownload, wameunganisha vipande Hersi, Kamwe, Privaldinho na Manara wakiwa wanamsifia Chama katika mazingira tofauti, kwamba ndio mchezaji bora kwenye ligi ya Tanzania kwa misimu yote aliyokuwepo hakuna anayemgusa
 
Mimi sinaga ushabiki maandazi, mbona simsemi ngoma, tshabalala na wengine, ukweli ni kwamba ngoma na baadhi ya wachezaji wanazingua kwa mazimgira tofauti, kibu nguvu nyingi akili kisoda
Ila kuna bad day kwenye kazi..huyu kibu ni msaada siku zingine..yani Simba inaongoza kwa kuwalaumu na kuwasema wachezaji wake..nadhani kama wanasomaga maoni waweza pata depression..
 
Back
Top Bottom