Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kuvurumishwa leo November 9, 2022 kwenye Uwanja wa Estadio de Liti mkoani Singida ambapo Walima Alizeti Singida Big Stars ambao ni wenyeji, wanamkabili vikali Mnyama Mkali Mwituni Simba SC
Mechi inatarajiwa kuwa ni ngumu sana na ya kusisimua kwa muda wote wa mchezo kutokana na kila timu kufanya maandalizi ya kutosha ili kuweza walau kupata ushindi dhidi ya mpinzani wake.
Timu zote zina alama 17 kwenye msimano wa Ligi Kuu lakini wakiwa nafasi tofauti kutokana na mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo basi tutegemee kuona ushindani wa kweli na burudani ya aina yake ndani ya dakika 90 za jasho na damu.
Kumbuka mchezo kwa saa za Afrika Mashariki ni kuanzia saa 10:00 Alasiri.. Usikose Ukapata Simulizi Jikite Hapa Hapa JF
...Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana...
==========
01' Kabumbu limeanza uwanja wa Liti, Singida
07' Phiri anafika lango la Singida, mpira unaenda pembeni ya lango. Goal kick.
09' Singida wanapata kona, inaingizwa kati bila kuzaa matunda
11' [emoji460] Deus Kaseke anaiandikia Singida bao la kwanza, Singida 1-0 Simba