FT: Tabora United 0-4 Simba SC | NBC Premier League | A.H.Mwinyi Stadium | 06.02.2024

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mkuu seriously. Siyo tu hapa mtandaoni. Hata kitaa. Nikiwa nimekaa hakuna mtu anajuwa mimi mshabiki wa timu gani, maongezi ya washabiki wa Yanga huwa yananishangaza. Yani ni watu wa tofauti sana. Ni wale wenye tabia halΔ±sΔ± za watanzania. Wenye kufuatilia mambo ya watu, wenye roho mbaya nk.

Fuatilia mkuu utagundua. Wanafuatilia Simba kuliko wana Simba wanavyowafuatilia. Saa nyingine wanajidai na wao ni SimbaπŸ˜€ kama yale ma ccm ambayo nayo saa nyingine yanajidai ni wapinzani eti wanatoa ushauri.

Ni wa tofauti sana kwenye hali ya kawaida ya ushabiki wa mpira wa miguu…Ni wananchi kweli wa hii nchiπŸ˜€
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Leo ndio wananishangaza zaidi yani!
Eti Tabora wameuza.

Uto hamnazo kabisa.
 
Goli alilofungwa kipa wa leo lilikuwa linataka kufanana na lile alilofungwa Diarra na Okrah (wakati ule akiwa timamu)

Ila hili la leo lina vitu vingi sana ndani yake (inahitaji uwe mtu wa mpira kuweza kujua)

Huwezi kumpa lawama kipa kwa kushindwa kudaka mpira ule (labda kama hujui mpira)

Maneno ya kwenye mabano ukishirikisha akili kuyasoma kiupembuzi utakuwa umenielewa (kitu ambacho nina mashaka nacho kuwa utaweza)
 
Anayeforce iwe hivyo ni Uto.
wala sio Tabora.

Tumewabakisha Azam tu sasa.

Mechi ya Kisasi.
 
Anayeforce iwe hivyo ni Uto.
wala sio Tabora.

Tumewabakisha Azam tu sasa.

Mechi ya Kisasi.
Mkuu naomba kuuliza, kwa hizi points walizotuzidi yanga na kwa mechi za ligi zilizobaki kuna uwezekano wa kuwapiku na kuchukua ubingwa, jana nilimind sana dodoma walivyowaachia zile points tatu saa hii tungekuwa tumepunguza gap yani
 
Mimi ni shabiki wa NYUMA MWIKO FC lakini inatosha kusema simba wapo vzr sn na hatuwawezi.
 
Kuna video inatembea ikionyesha jinsi Simba wanavyo mwaga unga (dawa) kabla ya mechi yaani hadharani bila woga .

Wakati uo wachezaji wa Simba wakiwa kwenye benchi lao wakijiandaa kupasha misuli moto.
Nilifikiri walijifunza kule South Africa kumbe Bado.
Aya mambo ndio Azam walikataa kufanyika katika uwanja wao na ndio sabau Simba wanahangaika kupata uwanja watakao ruhusiwa kufanya hivi.

Natumaini kwa muda ule wa tukio Match commissioner alikuwepo na Tukio lile litakuwa limeripotiwa katika ripoti yake ya mchezo
Hatutegemei kamati ya saa 72 kukalia kimya swala ilo maana Simba walisha liaibisha Taifa kule South Sasa niwakati wa bodi ya Ligi.
 
Kulingana na namna simba wamecheza mechi mbili hz za ligi vipi mnaona kama wamejipata au bado tuwape muda
Subilia ijumaa mechi na Azam ndio utajua kajipata ama kibunda kimefanya yake!
 
Unapotezaje mda kuandika pumba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…