Bora wangemchukua yule dogo wa yanga aliesajiriwa majuzi hapa shekhan kama sikosei, dogo ana ujasiri wa kupiga mashuti. Muda wa kufosi goli anapelekwa uwanjani anaweza akaotea moja ya maana, kwa kusema kweli viungo na washambuliaji sijaona hata mmoja aliepiga shuti la maana, cha kusikitisha zaidi sioni kizazi cha wafungaji wa kuokoa jahazi next afcon. Asilimia kubwa ya wachezaji watakua hawa hawa tu. Mabeki ukimtoa tshabalala ambae umri wake halisi una utata kidogo wengine wote watakua kwenye umri sahihi kwaiyo wakirudi hao hao sio mbaya ila kule mbele ndio sioni kizazi cha kuwa-replace samata na msuva. Next afcon tumaini letu litakua shekhan, yanga wamtunze vizuri yule dogo.