FT: Tanzania 0 - 3 Morocco | AFCON 2024 | San Pedro, Ivory Coast | 17.01.2024
Hapa kwangu mimi tatizo linakuja kwamba timu haina straika

Sisi kama watanzania tunakosa watu wabunifu pale mbele

Angalia pacome,chama,aziz ki, yule jamaa anachomekeaga yule wote ni 10 esque players wanaovuma nchini

Watu hatuna 9 mwenye nguvu
Hatuna namba 10 wenye ubunifu
Timu imejaa wakata umeme na mabeki kibao ambao hawatumii akili kubwa
Mwisho wa siku tunajitahidi kulinda ila kushambulia hamna kitu

Na bila magoli hamna ushindi
Ni kweli mkuu.

Ila ubunifu waanzia kwenye grass roots ambako wenzetu ndio wamewekeza.

Michezo kama mpira wa miguu sasa hivi ni lazima uwekeze fedha za kutosha na si zikitolewa kuzitumbua.

Wenzetu wamewekeza na sasa hadi watoto wa kike wana world Cup yao na huo ni uwekezaji.

Pia hawa wenzetu katika vyuo vikuu wana shahada mbalimbali za michezo.

Tunahitaji viongozi wa mpira wenye wabunifu, waso na tamaa na wenye kujituma.
 
Yani wanacheza taratiiiibu hawana haraka utafkiri wao ndo wanaongoza . Wanakera mno
 
Nyokaaa haondoki na nyama yako anakugonga anakichafua anaanza
 
hawa dawa yao tuwapige hata butii tu potelea mbali washinde cha moto wakione
 
Screenshot_20240117_210352_WhatsApp.jpg
 
Kiukweli mpira wanaocheza wachezaji wetu unashangaza sana pale wanapopoteza sana pasi bila sababu ya msingi....beki anapiga mpira mbele bila kujua anampigia nani

Pia Samatta anawachosha sana wenzie
 
Back
Top Bottom