Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuingia kucheza Mchezo wake wa kwanza wa AFCON dhidi ya Morocco kwenye mji wa San Pedro, Ivory Coast. Mechi hii itachezwa saa 2:00 usiku
Timu hizo zipo kwenye kundi F ambpo timu nyingine ni Zambia na DR Congo.
Upi utabiri wako wa mechi hiyo?
===========
Timu ya taifa ya #Tanzania ‘TaifaStars’ inatarajiwa kuanza ushiriki wake wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) kwa kukipiga dhidi ya Morocco katika mchezo wa Kundi F, leo Januari 17, 2024.
Baada ya mechi ya Morocco, Tanzania inayonolewa na Kocha Adel Amrouche inatarajiwa kukutana na Zambia (Januari 21, 2024) kisha dhidi ya DR Congo (Januari 24, 2024).
Jikumbushe historia ya mechi zilizopita baina ya wababe hao wawili; Tanzania 0-2 Morocco (2023), Morocco 2-1 Tanzania (2013), Tanzania 3-1 Morocco (2013), Morocco 3-1 Tanzania (2011), Tanzania 0-1 Morocco (2010).
View attachment 2874722
Dakika ya 29 Morocco 0 - 0
22' Himidi Mao anaoneshwa kadi ya njano
Dakika ya 30 Morocco wanapata goli la kwanza
31' Novatus anaoneshwa kadi ya njano.
Dakika ya 33 Morocco 1 -0 Tanzania
Dakika 38 anatoka Tarryn anaingia Msuva.
HT: Morocco 1 - 0 Tanzania
46' Anaingia Morice Abraham anatoka Mudathir