FT: Yanga 2-1 Red Arrows | Siku ya Wananchi 2024 | Mkapa Stadium

FT: Yanga 2-1 Red Arrows | Siku ya Wananchi 2024 | Mkapa Stadium

Mpira umeisha kwisha now ni muda wa WWE

Upande wa red arrow mechi inamuhitaji zaidi John Cena
 
Kwanini ali kamwe hajaonekana?😞😢
IMG_2665.jpeg
 

Sasa ni zamu Wananchi Yanga kuonyesha visu vyao. Jumapili hii Agosti 4 katika dimba la Benjamin Mkapa itakuwa ni kilele ya Wiki ya Mwananchi utambulisho wa wachezaji wa msimu wa 2024/2025 kufanyika.

Utambulisho huo utakamilishwa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Kagame Cup, Red Arrows kutoka Zambia.

=====

00' Kipenga kimepulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga 0-0 Red Arrows.

04' Red Arrows wanapata free kick ya kwanza kuelekea Yanga baada ya Boka kumdondosha Anthony.

06' ⚽ Rick Banda anaitanguliza Red Arrows kwa bao la mapeeema, ni mpira wa kichwa.

07' Almanusura Pacome airejeshe furaha ya wanayanga baada ya gonga kadhaa, juhudi zinashindwa kuzaa goli.

13' Aucho yuko chini baada ya kuwania mpira wa juu na Banda. Anarejea uwanjani baada ya kupata huduma ya kwanza.

15' Mzize anajaribu shuti kali kutoka nje ya 18 lakini mpira unapaa juuu ya lango la Red Arrows.

21' Yanga wanapata kona na kuianzisha chap chap, mipango yao inashindwa kufanikiwa.

24' Red Arrows wanapata kona mbili mfululizo, Diarra anauweka mikononi barabara.

25' Baleke anapata mpira maridhawa lakini filimbi ya offside inalia.

26' Yanga wanaumiliki mpira langoni kwa Red Arrows bila kupata bao.
Kuna jitu linauwawa huku
 
Back
Top Bottom