FT: Yanga 2-1 Simba | Yanga yatwaa Ngao ya Jamii

Na dalili ya kwamba hamna kitu mle angalia mzungu aliyemleta. Tizama hata sub zake! Hajui hata mtu kama chama anafanya nini uwanjani kuunganisha timu. Kiufupi simba mwaka huu tena imepigwa na kitu kizito.
Hivi viongozi hawa mafundi bomba wa rangi nyeupe huwa wanawatoa wapi?? Au ndio yale mambo ya tenpercent. kocha anabahatisha mpira kama kilimo cha nyanya
 
Simba mbovu acha kujifariji.
 
Mliposhinda kwenye bonanza hizi ngonjera hatukuziona,nyuzi zilijaa tele hapa JF mkisifu na kuabudu kana kwamba mmeotea dhahabu uchochoroni!.

Huu ni mwanzo tu Makolo nyie,mtapata taabu sana![emoji2][emoji2]
 
Ila huyu Inonga aache sifa za kijinga anaweza kutucost game kubwa kama zile za CAF.

Binafsi nalaumu sisi mashabiki, tunashangilia mchezaji akifanya mambo ya kipuuzi yasiyo na faida kwa timu.
Kungekua na VAR red card ingehusika leo
 
Kipindi cha kwanza Simba inaongoza goli moja na ball possession, Kocha akaona msinitanie...akamtoa Chama nje basi roho yake ikawa kwatu.
Acha kujutoa ufahamu CHAMA alipoteana kipindi cha pili na ametoka wakt wako 1-1 acha kujitoa ufahamu hapa.
 
Jamani Simba imeniumiza Sana ila tumpe muda kocha ila inauma japo ndio mchezo ila Kama shabiki wa Simba na Man u ndio wenge linapoanzia
Tatizo sio rangi, kwani rangi hiyo mmeanza nayo leo? Hiyo si mnatumia siku zote? Kilichowaponza ni jeuri zenu, kwa leo mlipopata goli kipindi cha kwanza mlitakiwa muwe wapole, sasa nyie kelele kibao, sisi wengine hatujazoea kelele, ndo ikabidi tupange mikakati ya ushindi ili kukata ngebe. Labda nikushauri kitu kimoja; ukitangulia na baiskeli la miti, usifikiri utawahi kufika, kuna phoenix nyuma yako inakuja. Halafu, ukimwona mtu kabeba begi, yawezekana anasindikiza tu, anayesafiri yuko nyuma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…