FT: Yanga 5-0 Zalan (Agg 9-0) | Caf Champions League | Mkapa Stadium | 17-09-2022

FT: Yanga 5-0 Zalan (Agg 9-0) | Caf Champions League | Mkapa Stadium | 17-09-2022

Wangekuwa wachovu wasingekuwa champions league
Champion league ina amuliwa kwa timu kuchukua ubingwa

Timu yao imechukua ubingwa ila ni ligi mbovu, kwanza imeanza around 2014 pili hata upinzani wao uwanjani unaweza kuona ni kiasi gani ni low

Angalia tu kwenye mpira wa mwisho wa moloko ambapo cross yake imeenda juu ya lango. Alikuwa amezungukwa na wachezaji watatu lakini wote wanamuangalia, hakuna aliyemfata kumzuia mpala jamaa anautuliza na kupiga shuti
 
Mchezo wa pili baina ya Yanga dhidi ya Zalan kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, leo Jumamosi Septemba 17, 2022, ni Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo wa kwanza Yanga ilishinda kwa mabao 4-0.

Kumbuka mshindi wa mchezo huu ataenda kukutana na mshindi kati ya Saint George ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.

Timu zimeshaingia uwanjani kwa ajili ya mchezo huu.
Mchezo umeanza...

10' Yanga wanatawala muda mwingi

18' Zalan wanaonekana kucheza kwa utulivu lakini muda mwingi mpira upo kwa wachezaji wa Yanga

45' Mpaka sasa Yanga imepiga jumla ya mashuti 11 ambayo hayajalenga lango la Zalan

45' Mashuti ya Yanga ambayo yamefika langoni mwa Zalan ni mawili

MAPUMZIKO: Yanga 0-0 Zalan

Kipindi cha pili kimeanza

46' Yanga wameendelea walioishia wanapiga pasi nyingi

GOOOOOOOOOOOOOOOO

47' Farid Musa anaipatia Yanga bao la kwanza
Farid amefunga kwa shuti kali akimalizia pasi nzuri ya Fei Toto.
50' Yanga wameongeza presha na wanafika langoni kwa Zalan mfululizo

56' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Azizi Ki anaipatia Yanga bao la pili

59' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Fiston Mayele anafunga bao la tatu kwa shuti la mbali, kipa anabaki anautazama mpira

62' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mayele anafunga bao la nne kwa Yanga

64' Yanga imetawala mchezo, wanapiga pasi muda mwingi na mpira wanaumiliki wao.

66' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mayele anafunga bao la tatu kwake na la tano kwa Yanga

76' Kasi imepungua kwa timu zote

80' Mayele anaomba kutoka baada ya kuumia. Anaonekana akishika sehemu ya nyuma ya paja

81' Mayele ametolewa uwanjani akichechemea
Kama unaona wameonewa ilete timu yako.
 
Back
Top Bottom