FT: Young Africans SC 3 - 0 Medeama FC | CAFCL | Benjamin Mkapa Stadium | 20.12.2023

FT: Young Africans SC 3 - 0 Medeama FC | CAFCL | Benjamin Mkapa Stadium | 20.12.2023

Ah wee, hiyo sahau.
😂😂 nashauri msije wengi!!
Yanga kwa Mkapa huwa hawashindi mashabiki wakiwa wengi.

Medeama ni black race pia, Saa kumi kwao hakuna challenge yoyote.

Jana Waarabu tuliwahenyesha, muda pia ulichangia ujue.
 
Hivi yanga mbona hawako serious yaani point 2 kweli jaman,, huu ni useng aisee
 
Sheria inawataka siku moja kabla ndiyo wafanye mazoezi kwenye uwanja utakaotumika kwa ajili ya mechi.

Nawapongeza wadau wote waliowafanyia hiyo hujuma ya kuwanyima uwanja wa mazoezi. Kwa hapa tulipofikia, siyo mbaya kumharibu kisaikolojia mpinzania wako, kupitia vitu vidogo kama hivi.
Ukiacha hiyo ya siku moja kabla, sheria inataka timu mwenyeji impatie uwanja wa mazoezi mgeni wake hata zile siku kadhaa kabla ya mechi. Mlishindwa kufanya hivyo na nadhani kuna faini inawahusu.
 
Mshindwe wenyewe tu!! Madeama hata kwenye 30 bora za Afrika haimo!! Na mkiiangusha ni sawa na kusukuma mlevi, msidai sifa yoyote!!
mbingunikwetu Mungu anakuona, mpaka wanacheza kwenye makundi lazima ujue kuwa wanajua, na vilevile ukumbuke wao ni mabingwa nchini kwao, ndiyo wapo njiani katika mchakato wa kuandika historia na kuwa kwenye hizo timu bora Afrika, hivyo usichukulie poa, usishangae Madeama miaka ijayo akawa miongoni mwa timu hatari, hivyo mechi usidhani itakuwa nyepesi, na kwa taarifa yako kundi la Yanga ni kundi gumu, kwani kila timu ni mshindi wa ligi nchini kwake. Hapa kinachotakiwa ni kuutumia vyema uwanja wa nyumbani.
 
Yanga ina timu nzuri Lakini inakuzwa mno kuliko uwezo wake.

Yanga ni watu wa Jihadi na ndiyo maana kauli mbiu yao ni "Daima mbele nyuma mwiko".

Miaka yote ushindi wao hutokana na kukamia mechi na siyo ubora wa kikosi chao.

Msimu wa mwaka Jana 2022/2023 walichukua ubingwa lakini kitakwimu Simba ilikuwa bora zaidi yao.

Hata Mayele anayekuzwa sana hajawahi kuwa mfungaji bora peke yake. Msimu wa 2021/2022 alizidiwa na George Mpole Lakini sifa alipewa yeye.

Kwa ivo Yanga ni timu nzuri ila haina huo ubora inayokuzwa nayo. Yanga ni mtambo wa Propaganda (Tanzania football Propaganda Machine) za mpira Tanzania.
 
Mimi mbona ndio naipasi hapa saa 7 tu niko uwanjani?
🤣😂🤣 Nitumie picha ukiwa viunga vya uwanjani ndiyo nitaamini.

Ila hold oooooon. Mnapiga pasi jezi zenu??? 😗😗
 
😂😂 nashauri msije wengi!!
Yanga kwa Mkapa huwa hawashindi mashabiki wakiwa wengi.

Medeama ni black race pia, Saa kumi kwao hakuna challenge yoyote.

Jana Waarabu tuliwahenyesha, muda pia ulichangia ujue.
Ngoja kwanza, hii mechi hakuna kuingia bila jezi ya Yanga, kwahiyo utavaa?

Yani katika vitu vya kipuuzi mtu akisema namdharau ni suala la jua sijui Waarabu hawawezi kucheza vizuri!

Like WTF? Mnafikiri hawalijui hilo? Hawafanyi mazoezi wakati wa jua kali?
Kwamba kwao hamna jua ndio wanakuja kulionea hapa?

Kwa takwimu za Wydad kwa sasa wameporomoka, sio ajabu kufungika.
 
Sawa, mnaichukulia Medeama poa sana.
Ni team inayocheza kwa mfumo wenu.

Wao wanakuja na lengo lao ni kujilinda.
Wao yanga utasikia tukimfunga medeama tunakua na point 5 then al ahly tutamfunga kule kwake tutafikisha points 8..... Halaf tena wale wa algeria kwa mkapa hawatoki hapo tutakua tunaongoza kundi na points 11. Yanga wao ni km uumbaji wa mungu yaani wakisema inakua hivyo...
 
Ukiacha hiyo ya siku moja kabla, sheria inataka timu mwenyeji impatie uwanja wa mazoezi mgeni wake hata zile siku kadhaa kabla ya mechi. Mlishindwa kufanya hivyo na nadhani kuna faini inawahusu.
Tutalipa tu. Muhimu malengo yaliyowekwa, yatimie.
 
Back
Top Bottom