FT: Young Africans SC 3 - 0 Medeama FC | CAFCL | Benjamin Mkapa Stadium | 20.12.2023

FT: Young Africans SC 3 - 0 Medeama FC | CAFCL | Benjamin Mkapa Stadium | 20.12.2023

Haya, Wanachi wenye nchi yetu ndio tunaingia sasa kutokea uwanjani.

Hivi kuna mtu bado anabisha kuwa Pacome ndio usajili bora zaidi kwa msimu wa 2023/24 Tanzania?

Hongereni Wananchi wenzangu na watani zetu wenye akili timamu waliotutakia ushindi kiroho safi.

B… Thanks, tokea jana, leo umesisitiza kututakia kheri & ushindi. Bless
Mdakuzi
Nyie leo itakuwa mmewaotea wale jamaa maana jinsi walivyokuwa wamejichokea ...ata kukokota mpira wanashindwa
 
Haya, Wanachi wenye nchi yetu ndio tunaingia sasa kutokea uwanjani.

Hivi kuna mtu bado anabisha kuwa Pacome ndio usajili bora zaidi kwa msimu wa 2023/24 Tanzania?

Hongereni Wananchi wenzangu na watani zetu wenye akili timamu waliotutakia ushindi kiroho safi.

B… Thanks, tokea jana, leo umesisitiza kututakia kheri & ushindi. Bless
Mdakuzi
Hongereni sana kwa jitihada na ushindi huu. Kikubwa mjue kwamba kuna kazi kubwa sana mbele kuliko ya kusaka ushindi leo.

Ova
 
Kigezo hapo sio goli tu la ugenini

Kigezo ni idadi ya magoli yaliyofungwa ugenini mlipokutana.

Yanga hajafunga goli lolote ugenini walipokutana na Cr Belarouzidad

Kwa kigezo hicho Yanga akiruhusu bao lolote akiwa nyumbani maana yake ametolewa licha ya idadi ya magoli atayopata
Duuh hizi sheria ni hatari
 
Hongereni sana kwa jitihada na ushindi huu. Kikubwa mjue kwamba kuna kazi kubwa sana mbele kuliko ya kusaka ushindi leo.

Ova
Mmeshaanza sasa, hamna jema nyie b…

Hayo kwani hatuyajui jamani? Unajua kama zile watu mmefiwa mpo msibani, mmejisahau kidogo mnakula mnafurahi anatokea mtu kuwakumbusha “Nyie kuleni tu, kesho tunazika”
Likeeeeee? Nani hajui hilo?
C’mon b…
 
Kwa first leg nilichokiona sitaki kuamini eti yanga leo atakuwa anajipigia hivyo itoshe kusema draw yaweza kuwa lakini pia kupigwa kunaweza kutokea .

Ila kwa muumba wangu ni yanga yamkute ya kumkuta .

Nenda Medeama mimi ni mghana toka zamani sana

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Baada ya mechi watu wanasema Medeama ni kama Ihefu tu. Wewe unasemaje mkuu?
 
Uto wanashambulia sana...wakitulia wanashinda.
Hapa ulishaanza kubadili msimamo wako juu ya "unyonge wa Yanga kwa Medeama" Poleni sana Simba. Yangu ni nzuri tena sana, kubalini tu. Acheni roho za korosho.
 
Mmeshaanza sasa, hamna jema nyie b…

Hayo kwani hatuyajui jamani? Unajua kama zile watu mmefiwa mpo msibani, mmejisahau kidogo mnakula mnafurahi anatokea mtu kuwakumbusha “Nyie kuleni tu, kesho tunazika”
Likeeeeee? Nani hajui hilo?
C’mon b…
Kitu huwa kinaponza timu zetu za soka, kwa kuanzia na timu ya Taifa, ni sherehe ndefu za ushindi wa awali. Hii ni mbaya.

Si unaona hata wewe umekasirika kukumbushwa majukumu, unataka sherehe itawale? Hii ndiyo kawaida yetu Watanzania.

Tunasheherekea mno hadi tunasahau majukumu yaliyo mbele yetu kwenye jambo hilohilo linalofanya tuwe katika sherehe hiyo.

Mna kazi kubwa zaidi mbele, kama ilivyo sisi ili kuwa sherehe kubwa zaidi.

Ova
 
Simba ingekuwa ndio inacheza na Madeama ingekuwa mbele goli tatu Hadi hivi Sasa!!!
Duuhh... wewe hata kwenye maisha ya kawaida unaonekana una roho ya korosho sana. Badilika, mwenzako akifanya kizuri pongeza tu.
 
Kitu huwa kinaponza timu zetu za soka, kwa kuanzia na timu ya Taifa, ni sherehe ndefu za ushindi wa awali. Hii ni mbaya.

Si unaona hata wewe umekasirika kukumbushwa majukumu, unataka sherehe itawale? Hii ndiyo kawaida yetu Watanzania.

Tunasheherekea mno hadi tunasahau majukumu yaliyo mbele yetu kwenye jambo hilohilo linalofanya tuwe katika sherehe hiyo.

Mna kazi kubwa zaidi mbele, kama ilivyo sisi ili kuwa sherehe kubwa zaidi.

Ova
Wala sikuwa nimekasirika, at all. Tena wakati najibu hiyo nilikuwa nacheka sana.

Sikiliza b... Binafsi huwa napenda nikiwa na cha kunifurahisha basi nikifurahie kwa nafasi, ukifika wakati wa majonzi nitahuzunika ila sio kwa kujinyima kufurahi wakati huo kwa kuwazia yajayo, lah!

Lakini mechi nyingine ni mpaka February mwishoni ujue? Muda upo wa kutosha kwa kufurahi na kufanya maandalizi.
Cheers
 
Back
Top Bottom