Jinsi uongozi wa Tanzania unavyoshughulikia masuala ya ufisadi ni ajabu ya aina yake. Kuna mambo mengi makubwa yaliyotokea huko nyuma lakini kumekuwa na ile mentality ya kuyaona kuwa ni upepo tu utapita, mentality ambayo kwa kiasi kikubwa imetokana na JK mwenyewe.
Pengine ni kweli, skando zote za Tanzania ni upepo tu utapita, na hakuna anakaefanya lolote.
Suala la Ndege ya Raisi wa China limekuwa Upepo tu umeshapita. Suala la Wanyama kutoroshwa pale KIA. Suala la Mgomo wa Madaktari. Suala la Fedha za EPA. Suala la wenye mamilioni ya fedha za ufisadi nje ya Nje ya Nchi. Suala la kutekwa, kuteswa au hata kuuwawa kwa waandishi wa habari na raia. Suala la Kukusanya hela kuwahonga Wabunge wapitishe bajeti ya Madini na Nishati, Uuzwaji UDA, Ufisadi Shirika la Reli, Migomo ya Walimu, Ufisadi ATC, nk, nk; yote yalikuwa ni upepo tu ukapita.
Sasa kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Zitto, PAC, kuwatimua na kuwafikisha Mahakamani watu wazito kama kina Pinda, Muhongo, Mboma nk, je, tutashuhudia tena, kama kawaida ya serikali yetu, ile dhana ya kwamba Escrow ni upepo tu utapita?
Yetu Macho.