Ni kweli Mkombozi Bank ni ya kanisa na moja ya dhambi katika kanisa ni wizi na udanganyifu. Ifahamike kwamba bank hii inaendeshwa sawa na bank zingine chini ya usimamizi na miongozo kutoka central bank.
Kama kuna statutory/regulatory requirements ambazo Mkombozi Bank haiku comply wakati wote wa kufunguliwa kwa accounts na kufanya hizo transactions in question, naomba ziwekwe hapa tujadili. Vinginevyo hatutatukuwa tukiwatendea haki tukiwahukumu kuwa ni wakosa wakati hakuna kosa lililobayana ambalo wao kama bank wamelifanya.
Kuhusu askofu Kilaini na mwenziye, ni kwwli fedha walipokea. Mwenye ushahidi kwamba ffedha hizo walizipokea kwa niaba ya kanisa ama kanisa liliwatuma kuwa na huo ubia, aweke hapa. Kinyume na hapo ifahamike kwamba Kilaini ni viongozi wa kanisa lakini wao si kanisa. Ndiyo maana sheria imebainisha ni wakati gani mtumishi atahesabiwa kafanya kosa la kikazi linalomhusisha mwajili anayemwakilisha, ni wakati gani anakuwa ame commit personal offence, hata kama ni mtumishi.
NINAOMBA TUZITENDEE HAKI DHAMIRA ZETU KWA KUCHAMBUA HOJA KATIKA MISINGI YA UKWELI SAHIHI BADALA YA EMOTIONS NA MISUKUMO YA UTASHI WETU.
Tuko pamoja.